Katika picha: Muonekano maridadi wa mwisho katika mradi wa upauaji wa haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kuongezeka kwa mazuwaru katika mwezi wa Muharam na Safar, wamerudi kuendelea na kazi ya upauaji wa uwanja wa haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s) ikiwa ni awamu ya mwisho, inayo husu kufunika paa la pili kwa upande wa ndani pamoja na kuweka viambatanishi vyake (mapambo), na maraya (madini ya vioo) na hasa katika upande wa mlango wa Qibla katika haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s), kwani paa la upande huu linatofautiana na pande zingine kutokana na umuhimu wa sehemu hii.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya ambao ndio wasimamizi wa mradi, muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh alisema kua: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa na kitengo cha miradi, sehemu inayo jengwa kwa sasa inahitaji muda zaidi na umakini mkubwa kwanza eneo lake ni pana na lipo juu zaidi kuliko maeneo mengine ya paa hili, shirika linalo tekeleza mradi huu ni: (Shirika la aridhi tukufu la kihandisi na ujenzi), hawajapunguza juhudi, wamekua na hamu kubwa ya kukamilisha mradi huu ambao baada ya kukamilika utatoa muonekano wa aina yake katika haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s).

Akaendelea kusema kua: “Sasa hivi mtu anaye kuja kufanya ziara anaweza kushuhudia kwa macho yake kuendelea kwa kazi za mwisho katika upauaji huku likianza kuleta muonekano wake kidogo kidogo, hakika mradi huu enaenda vizuri na watumishi wote wanafanya kazi kwa bidii sana, wana hamu kubwa ya kukamilisha kazi hii inayo enda kwa kufata uwiano wa kazi zingine za mradi wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kua: “Maraya (madini ya vioo) yanayo wekwa katika paa na sehemu zingine yametoka katika nchi ya Beljika ni aina bora kabisa ujazo wake ni milimita (2), pia rangi zake ni nzuri na ni imara, na huwekwa kwa kutumia gundi maalumu ya (CNC) na hukatwa kwa kutumia vifaa maalumu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliwapa (shirika la aridhi tukufu la kihandisi na ujenzi) ambalo ni shirika la kiiraq lenye makao makuu yake hapa Karbala, jukumu la upanuzi wa haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s) pamoja na upauaji, na ndipo shirika la (Aridhi tukufu) likaanza kutekeleza mradi huu kuanzia mwanzo kabisa, kuweka msingi, njia za umeme, njia za maji na shughuli zingine nyingi zenye uhusiano na mradi, jukumu la kukubaliana na mashirika ya kigeni kwa ajili ya kazi maalumu hufanywa kwa kuwasiliana na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi huu unafanywa chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: