Kundi la shamba boy wa Alkafeel wachambulia miti katika barabara za mji mtukufu wa Karbala..

Maoni katika picha
Kikundi cha shamba boy wa Alkafeel walio chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kazi ya kuchambulia miti iliyopandwa pembezoni mwa njia na barabara za mji wa kale wa Karbala tukufu, pamoja na ile iliyopo katika maeneo ya wazi, ambayo ilipandwa siku za nyuma katika mradi wa upandaji wa miti ambao hufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kua miti mingi ya maua iliharibika kibindi cha ziara ya mwezi wa Muharam na Safar, miongoni mwa kazi walizo fanywa ni:

Kwanza: Kuchambulia miti kwa umaridadi na ujuzi mkubwa ili kuifanya iwe katika muonekano mzuri.

Pili: Kuondoa miti iliyo haribika na kupanda mingine katika sehemu hizo.

Tatu: Kuandaa sehemu za kupanda miti na kuipanda kwa mpangilio.

Nne: Kusamadia miti hiyo.

Tano: Kupanda miti katika barabara zinato hitajia kuongezwa miti.

Kumbuka kua kazi hizi ni sehemu ya mradi wa shamba boy wa Atabatu Abbasiyya tukufu, jukumu lao ni kupanda miti katika mji wa Karbala mtukufu na kuhakikisha wanaupendezesha mji wa Sayyid Shuhadaau (a.s) hadi uwe katika muonekano bora zaidi uendane na heshima uliyo nayo katika nyoyo za waislamu duniani, miti yote ya mapambo na maua iliyopo ni sehemu ya kazi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: