Chuo kikuu cha Dhiqaar chaizawadia Atabatu Abbasiyya tukufu nakala mbili za maandishi ya kale na chasisitiza kua wao wanahaki zaidi ya kuhifadhi nyaraka za kale.

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Dhiqaar kikiwakilishwa na mkuu wa kitivo cha lugha Dr. Jaabir Muhsin Rikaabi kimeizawadia Atabatu Abbasiyya tukufu nakala mbili za thamani, ambazo ni miongoni mwa athari za zamani, ya kwanza ni nakala ya msahafu mtukufu ambayo inazaidi ya miaka 250 maandishi yake yameandikwa kwa maji ya dhahabu na yamepambwa kwa nakshi nzuri sana za kipindi hicho.

Nakala ya pili ni zaburi ya watu wa nyumba ya mtume, ambayo ni sahifa sajadiya ambayo kutokana na maandishi yake inakadiriwa kua na umri wa zaidi ya miaka 400.

Hayo yalifanyika pembezoni mwa ziara iliyo fanywa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika chuo hicho, ulio ongozwa na Dr. Zamaan Abedi pamoja na jopo la washauri wa jarida la turathi za Karbala kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu kuendesha nadwa za kitamaduni zitakazo zungumzia turathi za Iraq kwa ujumla na za mji wa Karbala mtukufu.

Dokta Jaabir Muhsin Rikaabi, wakati akikabidhi zawadi ya nakala hizo alisema kua: “Kilicho tusukuma kuwazawadia nakala hizi; hakika tumeona kua Atabatu Abbasiyya inastahili zaidi kuhifadhi nakala hizi, kwa sababu inatunza nakala za kale na inazitilia umuhimu na ina watu wenye uzoefu walio bobea katika kutunza nakala (athari) za kale”.

Akabainisha kua: “Nakala hizi tulizikuta katika duka la vitabu, tukazinunua kwa ajili ya kuzihifadhi, hakika watu wengi hawafahamu thamani za nakala za kale ili wazihifadhi au wazipeleke sehemu ambayo zinaweza kuhifadhiwa kitaalamu kwa njia za kisasa”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inamiliki kiasi kikubwa cha nakala za kale, ambazo zinarejea katika miaka tofauti, na imeajiri watu maalumu waliosomea mambo ya kale kwa ajili ya kuzirepea na kuzitunza, na wamepiga hatua kubwa katika jambo hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: