Baada ya kufaulu kwa uzoefu wa kuanzisha chuo na kufungua hospitali ya rufaa: Atabatu Abbasiyya tukufu imekusudia kufungua chuo cha udaktari na uuguzi katika mkoa wa Karbala tukufu.

Maoni katika picha
Uzoefu wa kufungua chuo cha masomo ya kibinadamu katika mji wa Najatu mtukufu unachukuliwa kua jambo la mafanikio lililo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika nyanja ya elimu ya juu, kutoka na hazina ya wasomi wa kisekula iliyo nao imeweza kuipatia jamii ya Iraq viwango vya kimataifa katika mambo inayo fundisha.

Baada ya kufunguliwa kwa hospitali ya Alkafeel katika mji wa Karbala mtukufu mwaka mmoja na miezi miwili iliyopita, na kupata ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma zake, imekua sawa na msingi katika kujenga nyumba za chini zitakazo tumika kama chuo cha udaktari.

Hivyo Atabatu Abbasiyya imekusudia kuifanya hospitali hii kua sehemu ya kujifunzia udaktari, kutokana na maelekezo ya waziri wa elimu ya juu na utafiti, aliye tembelea hospitali hiyo akiwa na jopo la watalamu, wakiongozwa na mkuu cha kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Nahrain pamoja na rais wa kamati ya wakuu wa vyuo vya udaktari vya Iraq Dokta Alaau Ghina Hussein, Atabatu tukufu ilionyesha nia yake ya kufungua chuo cha udaktari na uuguzi katika mji wa Karbala mtukufu.

Wageni walitembelea sehemu mbalimbali za hospitali ya rufaa ya Alkafeel ili kujionea utendaji kazi wa vitengo mbali mbali vya madaktari na wauguzi na kushuhudia vifaa tiba walivyo navyo pamoja na uwezo wa wataalamu wao ili kujiridhisha kama wanasifa ya kua walimu wa udaktari na uuguzi.

Baada ra ziara yao, walifurahishwa sana na uwezo mkubwa iliyo nao hospitali na ubora wa huduma inazo toa na hivyo ndio vichocheo vikubwa vitakavyo sababisha Atabatu Abbasiyya tukufu ikubaliwe kufungua chuo cha udaktari na uuguzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: