Kitengo cha mipango na maendeleo ya binadamu chakamilisha kozi ya ubora kwa watumishi wa Mudhifu (chakula) cha Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha mipango na maendeleo ya binadamu kimekamilisha kozi ya ubora kwa watumishi wa kitengo cha mudhifu (chakula) cha Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo lenga kuongeza viwango vya watumishi na kuwafanya waweze kutoa huduma bora zaidi.

Kozi ilifanyika katika ukumbi wa Mudhifu (chakula) ilijikita zaidi katika kuelimisha jinsi ya kuboresha huduma, na yalizungumziwa mambo mengi yanayo husu nyanja hiyo.

Mkufunzi wa kozi bwana Farasi Abdurazaaq Shimriy ambaye ni mtumishi wa kitengo cha mipango na maendeleo ya binadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alifafanua kua: “Kozi ya ubora imetolewa kwa watumishi wa kitengo cha mudhifu (chakula) cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuboresha huduma zaidi hadi kufikia kiwango cha juu katika nyanja tofauti, kama vile; namna ya kunyayua chakula na kukitenga mezani, na usafishaji wa meza, kila kitu kina namna yake ya utendaji”.

Washiriki walionyesha kufurahia kozi hii na wakasema kua; hakika imewaongezea ujuzi na wamenufaika sana na elimu waliyo ipata kuhusu fani hii.

Hii kozi ni miongoni mwa kozi nyingi, nadwa na warsha ambazo hufanywa kwa watumishi wa vitengo mbalimbali vya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuongeza viwango vyao vya elimu na ubora katika utendaji wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: