Sayyid Swafi: Hakika kila umma huonyesha historia yake kutokana na maendeleo ilio nayo sasa hivi au wakati wa nyuma..

Maoni katika picha
“Mwafahamu hakika kila umma huonyesha historia yake kutokana na maendeleo ilio nayo sasa hivi au wakati wa nyuma, pamoja na kua watu wengi wameishi hapa duniani hawapewi umuhimu wowote katika historia, wanao pewa umuhimu ni wale tu waliokua na vitu vya kuonekana katika jamii, sawa iwe ni katika uwanja wa elimu au mambo mengine yenye athari katika jamii, huvyo umma hujulikana kwa utendaji wao wa kazi, hata umma wa sasa unajaribu kuonyesha katika baadhi ya mambo kua hawakubaki nyuma katika maendeleo ya zamani”.

Haya yalisemwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyd Ahmadi Swafi (d.i) alipo hudhuria kongamano la kujadili uhalisia wa kimalezi na kielimu hapa Iraq, ambalo liliandaliwa na Maahadi turathi za mitume (a.s) na maomo ya hauza kwa njia ya mtandao, jioni ya siku ya Ijumaa (30 Rabiul Awwal 1438 h) alieleza mbele ya ujumbe wa idara ya malezi ulio shiriki katika gongamano hili, matatizo yanayo ikumba Iraq katika swala la elimu.

Katika khutuba yake alisema kua: “Watu wa Iraq wanajulikana kwa ukarimu, wanajulikana kwa utoaji, unapo fika wakati wa ziara ya arbainiyya (arubaini ya imam Huseein a.s) huonekana utukufu wa watu hawa na ukarimu wao, hujitolea mali na nafsi zao, kwa kufanya hivyo, sasa hivi tunapo zungumzia ukarimu wa wairaq tunao ushahidi”.

Akaendelea kusema kua: “Sisi hapa Iraq tunafahamu kua; toka zamani tulikua ni jamii yenye maadili mema na maendeleo mazuri, tuna mchango mkubwa katika historia, na leo tunakabiliwa na matatizo, kawaida yetu hatutaki kukaa na matatizo, yatakiwa tuyamalize, mwanadamu anaeishi miaka sitini au sabini, ataulizwa kuhusu miaka hiyo (thamani ya kila mtu ni kwa mazuri yake)”.

Akasema: “Sisi tupo mbele ya mapandanjia na kila njia inatuhitaji, hatuwezi sema tumetekeleza wajibu wetu, sasa hivi Iraq ipo katika kipindi kigumu, inatakiwa kila mmoja wetu ajitolee kwa juhudi zake zote, kila mtu ahisi majukumu, uhisi kuwajibika kama muiraq, uhisi kuwajibika katika kulea jamii na yatupasa tufikirie kuingia katika utendaji, mwanadamu ambaye sio mtendaji anakua sawa na mtu aliye jitenga”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: