Maahadi ya turathi za mitume (a.s) iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu yaendesha kongamano la kujadili hali ya masomo ya Iraq..

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za mitume (a.s) na masomo ya hauza kwa njia ya mtandao iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya siku ya Ijumaa (30 Rabiul awwal 1438 h) sawa na(30/12/2016 m) iliendesha kongamano lenye kauli mbiu isemayo: (Baina ya matatizo ya kijamii na matarajio ya baadae) ambapo ilijadiliwa hali ya malezi na elimu ya Iraq. Kongamano lilifanyika katika ukumbi wa imam Hassan (a.s), kongamano lilihusisha shule (50) za kitongoji cha Karakh na Sha’alah ambazo ziliwakilishwa na walimu mia moja, lilifunguliwa kwa kisomo cha Qur an tukufu, iliyo somwa na Muhammad Habibu kisha ikasomwa suratul Hamdu kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq kisha ikaimbwa qaswida ya (Ibaa) ambayo ni maalumu kwa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alihudhuria kongamano hili na katika khutuba yake alisema: “Mwafahamu hakika kila umma huonyesha historia yake kutokana na maendeleo ilio nayo sasa hivi au wakati wa nyuma, pamoja na kua watu wengi wameishi hapa duniani hawapewi umuhimu wowote katika historia, wanao pewa umuhimu ni wale tu waliokua na vitu vya kuonekana katika jamii, sawa iwe ni katika uwanja wa elimu au mambo mengine yenye athari katika jamii, hivyo umma hujulikana kwa utendaji wao wa kazi, hata umma wa sasa unajaribu kuonyesha katika baadhi ya mambo kua hawakubaki nyuma katika maendeleo ya zamani”.

Kisha ilifatia khutuba ya ugeni wa idara ya malezi iliyo somwa na Ustadhi Khamisi Aluwani Zaghbiy iliyo elezea hali ya elimu kwa sasa na uzembe wa viongozi wa serikali katika nyanja za malezi, alisema kua: “Badala ya kua na malezi yenye kumvutia mwanafunzi, tumekua na malezi yanayo futa ndoto za mwanafunzi, haya yanatokea kwa sababu ya mazingira ya kiuchumi, kijamii na kisiasa tunayo yapitia kwa sasa, swala la kimalezi hutegemea vitu fulani kama vile; shule, mwalimu, mwanafunzi, selebasi na usimamizi wa mambo, kwa sababu ya mapungufu ya viongozi na uchache wa shule kumesababisha kutokea matatizo mengi katika shule na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi, hadi kufikia wanafunzi (100) ndani ya darasa moja, mwalimu anapuuzwa hana lolote, hakuna mtu anaye mtetea na kumlinda kutokana na mafisadi, tunaomba ofisi za Marjaa mkuu ziingilie swala hili hasa wakati wa kupiga kura ya kulinda taasisi za kimalezi na kielimu”.

Kongamano liliendelea kujadili matatizo ya walimu na aliongea kiongozi wa Maahadi katika tawi la Sha’ala ambaye alisema kua: “Shukrani zangu za dhati nazielekeza kwa walimu wa tawi la Sha’ala walio chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) kwa juhudi kubwa wanazo fanya, tunahitaji uangalizi maalumu katika mji huu ulio dhulumiwa na unao umwa na hasa katika nyanja ya malezi, na ninamuomba kiongozi wa kisheria na viongozi wengine msaidie katika kupitishwa kwa sheria, kwa sababu uonevu kwa walimu umefikia kiasi ambacho haulezeki”.

Kisha aliongea dokta Mushtaqu Abbasi msaidizi wa kitengo cha malezi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, aliongelea mafanikio ya Atabatu Abbasiyya katika upande wa kielimu, na akadokeza kuhusu ufunguzi wa chuo cha udaktari wa binadamu kama mfano pamoja na ujenzi wa nyumba za chuni za chuo hicho kitakacho kua chini ya hospitali ya Alkafeel.

Naye muwakilishi wa Marjaa mkuu katika kitongoji cha Sha’ala Shekh As’adi Zubaidi alisema: “Tunatakiwa kutengeneza mtu mwenye kujitambua na mwenye juhudi, tunatakiwa kutengeneza familia njema na nchi imara, hivyo tunatakiwa kuwa na taasisi imara za malezi”.

Shekh Hussein Turabi kiongozi wa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) na masomo ya hauza kwa njia ya mtandao aliiambia Alkafeel kua: “Tumeona kua elimu inatoka katika msitari wake wa asili, na sasa hivi kuna matatizo mengi katika upande wa wanafunzi hali kadhalika upande wa selebasi na hata upande wa walimu, kongamano hili ni la kujadili mambo muhimu yanayo weza kumpa nafuu mwalimu pamoja na kujadili changamoto za elimu kwa ujumla, imefikia kiwango shule yenye uwezo wa kubeba wanafunzi (500) inakua na wanafunzi hadi (2000) jambo hili linaua elimu hapa Iraq, ndio maana swala la elimu limeanza kuelekea katika shule za binafsi, hili ni tatizo kubwa kwa familia ambazo hawana uwezo wa kulipa gharama za masomo katika shule binafsi, hii ni awamu ya kwanza ya Maahadi katika kitongoji cha Karakh, inshallah awamu ya pili itakua katika kitongoji cha Raswafah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: