Kwa kutumia picha za Faxmeil (Mukhtasar maraasimul alawiyyah) kitabu cha muhakiki Swadr kutoka kituo cha Hillah kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu..

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hillah kilicho chini ya kitengo cha maarifa za kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wametoa kitabu cha (Muhtasar maraasimul alawiyyah) cha muhakiki Hilliy (676 h).

Kitabu kimehakikiwa, na Ustadhi Ahmad Ally Majid Alhilliy kupitia chapa ya Nafisa iliyopo katika maktaba ya imam Kaashifu Alghitwaa , iliyo andikwa na mwanafunzi Sayyid Muhammad bun Mutrafu Alhasaniy (672), na hii ni sehemu ya majukumu ya kituo hiki, kuhakiki na kuchabisha vitabu vya kale katika kava jipya.

Kimechapishwa katika juzuu mbili, la kwanza: kitabu cha muhakiki na la pili nakala ya picha za Faxmeil, nao ni upigaji picha wa kisasa wa nakala za kale, umefanywa kwa mara ya kwanza hapa Iraq.

Kitabu kina sehemu zifatazo,

Kwanza: utangulizi wa muhakiki, una kurasa mia moja; utangulizi umeshiba, muhakiki wa kitabu kaelezea kuhusu Maraasimul Alawiyya (vikao vya ma’alawi) na nakala ya muhtasari pamoja na ruhusa (ijaza) zake, utangulizi huu umemaliza baadhi ya matatizo ya kielimu kwa baadhi ya wanazuoni wa Hillah.

Pili: kitabu chenyewe, na kina kurasa (110) ni maelezo halisi na milango ya kitabu cha Maraasimu.

Tatu: yaliyomo, imechukua kurasa (40).

Nne: picha za Faxmeil, ambazo ni picha za kitabu halisi pamoja na nakala ya Sharaai’I ya Ibun Baabawaih ukizingatia wao ni sawa na kitu kimoja kutokana na umuhimu wao, kitabu kimechapishwa katika juzuu mbili: juzuu la kwanza, ni kitabu cha muhakiki na la pili ni nakala za picha za Faxmeil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: