Waziri wa afya msaidizi kutoka Iran: Hospitali ya Alkafeel ni alama yenye kuangazia taasisi za afya za Iraq..

Maoni katika picha
Waziri wa afya msaidizi kutoka Iran dokta Imami Ridhwawi amesema kua Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni alama (taa) yenye kuangazia taasisi za afya na tiba za Iraq, na sisi tupo tayali kushirikiana nayo.

Aliyasema hayo alipotembelea Hospitali hiyo akiongozana na, Rais wa chuo kikuu cha Tehran katika kitengo cha tiba, dokta Jafari Yaan, Rais wa kitengo cha upasuaji wa chuo kikuu cha Iran dokta Baqaaiy, Rais wa chuo kikuu cha udaktari cha Shahid Bahashti dokta Afshaar na daktari bingwa wa upasuaji pamoja na wajumbe kutoka wizara ya afya waliokuja Iraq kutembelea Hospitali ya Alkafeel, ugeni huo uliongozana na dokta Haidari Bahadaliy katika kutembelea vitengo vya hospitali pamoja na vifaa tiba.

Hali kadhalika ugeni huu ulikutana na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) naye aliwaambia kua: “Hospitali ya rufaa Alkafeel bado inaendelea kujijenga kwa ajili ya kutoa huduma bora za matibabu, na imepiga hatua katika swala hili, Hospitali imepokea madaktari bora walio bobea katika fani mbalimbali kutoka sehemu tofauti, walio tayari kutoa mchango wao kama walivyo kua wakiwahudumia watu wao kuho waliko kua, pia Hospitali imeweza kuonyesha vipaji na uwezo wa madaktari wa ndani na nje ya nchi, na milango yetu ipo wazi kumpokea daktari bingwa yeyote mwenye ikhlasi na utayari wa kufanya kazi na sisi kwa nia ya kufikia lengo ambalo ni kuchangia katika kupunguza matatizo ya kiafya kwa raia wa Iraq na iondoe upungufu uliopo katika taasisi za afya za Iraaq”.

Ujumbe wa madaktari kutoka Iran ulionyesha kufurahishwa kwao na Hospitali ya rufaa Alkafeel, na hazina waliyo nayo ya vifaa tiba vya kisasa vinavyo endana na watalamu wao, na wakasema kua wapo tayari kushirikiana katika maswala ya tiba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: