Paa la uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) lina kubba za aina mbili, kuna kubba ndogo (14) zina upana wa nita tano (5) na urefu wa mita tatu (3) na aina ya pili ni kubba kubwa ambazo zipo nne, kila moja ipo usawa na nguzo ya uwanja wa haram tukufu, zina upana wa mita tisa (9) na urefu wa mita tano (5).
Kutokana na kubadilika badilika kwa hali ya hewa ya Karbala tukufu, na kwa ajili ya kulinda muonekano wa kubba hizi ambazo zimepambwa kwa Kashi Karbalai na viambatanishi vingine, watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wameweka utaratibu maalumu wa kukagua sehemu zote za Ataba tukufu na uangalizi wa kitalamu wa hizi kubba.
Mwanzoni mwa kazi hii Kubba zimesafishwa na kurudishiwa michoro yake kadri ilivyo hitajika kwa kila kubba.
Kumbuka kua kitengo hiki tayari kimekagua maeneo yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ni zaidi ya (170) katika vitengo vyake mbali mbali, na kuna kamati maalumu ya kuandaa fomu za mapendekezo, katika maswala ya majengo, umeme, makenika na mengineyo, fomu hizo hubainisha uharibufu uliopo katika katika eneo lililo kaguliwa ili mafundi wa kitengo husika wakarekebishe.
Tunapenda kukumbusha kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo vyenye kazi nyingi, vile vile kina idara nyingi na watumishi wengi, wanafanya kazi usiku na mchana katika maeneo mbali mbali ya Ataba tukufu.