Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika kongamano la Ataba na Mazaru takatifu..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwakilishwa na mwanachama wa kamati ya viongozi Sayyid Adnani Mussawiy imeshiriki katika kongamano la Ataba tukufu na Mazaru takatifu za Iraq, Iran na Sirya lililo fanyika katika Atabatu Radhawiyya tukufu na kudumu siku mbili mfululizo. Kongamano ambalo limehudhuriwa na viongozi kutoka katika Atabatu Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiya , pamoja na viongozi kutoka katika Mazaru matakatifu, hali kadhalika alihudhuria katibu mkuu wa Ataba na Mazaru za Iraq, wakiwemo wawakilishi wa Ataba na Mazaru tukufu za Iran na Sirya.

Kongamano hili ni kwa ajili ya mapendekezo na makubaliano yaliyo pitishwa katika kongamano la kwanza, na kuangalia mambo yaliyo fanyiwa kazi, ikiwepo kujadili mapendekezo mapya yatakayo wasilishwa katika kongamano lijalo litakalo fanyika katika Atabatu Husseiniyya tukufu, hali kadhalika kukamilisha uteuzi wa kamati kuu itakayo fatilia utekelezaji wa makubaliano yanayo fikiwa katika makongamano na kusimamia kamati ndogo ndogo, pamoja na kuunda kamati itakayo andaa kanuni za ndani kwa kamati zote, ikiwa ni pamoja na kuunda kamati tano kila moja ikiwa na majukumu maalumu.

Mwisho wamekubaliana wana kongamano kufikisha maelekezo yaliyo pasishwa katika kongamano hili kwa viongozi wakuu wa Ataba na Mazaru tukufu, kwa ajili ya kuyajadili katika kongamano lijalo, hali kadhalika muafaka wa kutolewa kitabu cha umoja kitakacho tolewa na Ataba zote pamoja na Mazaru matukufu kwa ajili ya kuwahudumia na kuwaongoza mazuwaru (watu wanao kuja kufanya ziara), na kuanzisha mtandao wa pamoja kwa lengo la kurahisisha mawasiliano na kubadilishana maoni ya kielimu na kitamaduni na kiutumishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: