Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza ratiba ya msafara wa Saaqi unaoelekea katika ibada ya Umra na kuzuru kaburi la mtume (s.a.w.w) na maimamu wa Baqii (a.s) na sehemu zingine tukufu katika mji wa Maka na Madina Munawara katika mwaka wa (1438 h), Ratiba itakua kama ifatavyo:
Siku ya kwanza: Wasafiri wote wakutane Mar aabu Saaqi barabara ya Maitham Tammaar kisha wataelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kwenda Jida, makazi yatakua katika mji wa Madina, watalala katika moja ya hoteli za mji huo.
Siku ya pili: kutembelea msikiti wa mtume mtukufu, kama muda ukitosha tutatembelea maimamu wa Baqii (a.s).
Siku ya tatu: tutatembelea maeneo matukufu ya Madina (Mashahidi wa Uhudi, Masjidi Qiblataini, Misikiti Saba, Masjidi Kuba na Mudhifu (sehemu ya chakula) ya imam Hassan (a.s)).
Siku ya nne: Siku huru (hakuna ratiba).
Siku ya tano: asubuhi ipo huru (haina ratiba) Safari itaanza baada ya Adhuhuri kuelekea Miqaat kwa ajili ya Ihraam, na tutaondoka baada ya Magharibi kuelekea Maka tukufu, baada ya kufika watu watapewa vyumba vya kulala.
Siku ya sita: Kutekeleza ibada ya Umra.
Siku ya saba: Siku huru (haina ratiba).
Siku ya nane: Tutatembelea maeneo matukufu ya Maka (Mlima Thuur, Arafaat, Muzdalifa, Minna, Mlima Nuur na makabuli ya Hajuun).
Siku ya tisa: Ibada ya Umra kwa niaba, kwa watakao penda.
Siku ya kumi: Siku huru (haina ratiba).
Siku ya kumi na moja: Kurudi katika nchi yetu kipenzi, tunatarajia kufika salama Inshallah.
Mambo utakayo fanyiwa katika safari ni:
1- Viza.
2- Makazi siku nne katika mji wa Madina na siku sita katika mji wa Maka tukufu.
3- Kutembelea maeneo matukufu katika mji wa Madina na Maka tukufu.
4- Usafiri wa kutoka uwanja wa ndege wa Jida hadi Madina na kutoka Madina hadi Maka kisha kutoka Maka hadi uwanja wa ndege wa Jida.
5- Msafara utaongozana na kiongozi wa kiofisi pamoja na mtoaji maelekezo ya kidini.
6- Kutakua na milo mitatu kila siku na ratiba ya chakula itakua wazi kwa wote.
Kwa maelezo na oda ya safari: Wasiliana na kitengo cha kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu kilichopo mlango wa Bagdadi katika jengo la imam Hassan Askariy (a.s) (hoteli ya Dallah ya zamani), au piga simu kwa namba zifuatazo (07801952436) na (07602283026).
Gharama ya safari kwa mtu mmoja ni kama ifuatavyo: Usd (875) kwa malipo ya keshi na Usd (950) kwa malipo ya kidogo kidogo (mkopo). Mtoto wa miaka 2 hadi 11 ni Usd (450) keshi na Usd (550) mkopo (kwa kulipa kidogo kidogo). Na kwa mtoto wa chini ya miaka 2 yaani ambaye bado ananyonya ni Usd (150). Kwa anaye taka mkopo lazima apate udhamini kutoka kwa mtumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pia atatakiwa kulipa kiasi cha Usd (200) na kiasi kitakacho baki kitakatwa kutoka katika mshahara Usd (100) kila mwezi.
Mkopo wa mtoto wa miaka 2 hadi 11, atatakiwa kutanguliza Usd (100) na kila mwezi atakatwa Usd (50).
Kwa kila anayetaka kwenda Umra, awasilishe paspoti yake iwe na zaidi ya miezi sita ya kuendelea kutumika na kopi ya kitambulisho cha uraia pamoja na picha tatu zenye (back ground) nyeupe.