Kumalizika kwa kozi ya kwanza kuhusu namna ya kuandika tafiti kuhusu Qur an (katika mwenyendo wa vizito viwili)..

Maoni katika picha
Kituo cha Maarifa ya Qur an tukufu na kuifasiri kilicho chini ya kitengo cha Maarifa ya kiislamu na kibinadamu kimemaliza kozi yenye anuani isemayo: (namna gani utaandika utafiti kuhusu Qur an katika mwenendo wa vizito viwili), nayo ni miongoni mwa kozi za kitaalamu ambazo huendeshwa na kituo hiki. Inalenga kuwasaidia watafiti na waandishi wa mambo ya Qur an namna ya uandishi bora kwa kufata mwenendo wa vizito viwili, katika kozi hii wametajiwa zana zinazoweza kumsaidia mtafiti katika kukusanya fikra za kitafiti na kuziwasilisha kutokana na utafiti wake.

Kozi ilifanyika katika ukumbi wa imam (Qassim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ilihusisha watafiti na watu muhimu katika uandishi pamoja na wanafunzi wa hauza.

Daaru Diffah, ulikua ni muhadhara wa Shekh Dhiyaau Diin Azubaidiy mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha, alielezea mambo ya msingi katika uandishi wa utafiti na kanuni maarufu za kielimu katika nyanja hii, kabla ya kuingia katika mada yake kwa kina alisisitiza kuhusu nafasi ya vizito viwili (Qur an na watu wa nyumba ya mtume watakasifu) ya kwamba ndio njia pekee inayo okoa kwa maelekezo ya mtume (s.a.w.w) katika haditi mashuhuri ya Thaqalaini (vizito viwili) ambayo ni Mutawatiri na sahihi, kisha akaelezea mwenendo wa vizito hivyo na namna ya kunufaika navyo kwa undani zaidi.

Washiriki walitoa shukrani nyingi kwa waandaaji wa kozi hii muhimu, wakasema kua wamepata mambo mengi ya msingi kuhusu mwenendo wa vizito viwili vitukufu, na walitoa sifa kem kem za kozi hii na wakaomba kuendeleza mwenendo huu mzuri.

Tunapenda kusema kua; Kitengo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha kitafanya kozi nyingine itakayo husu namna ya kunufaika na mwenendo wa vizito viwili vitukufu, kutokana na maombi ya watafiti, pia kituo kimeandaa anuani maalumu ya kupokelea maswali kuhusu mashindano ya (muandishi bora kuhusu Qur an tukufu katika mwenendo wa vizito viwili), Email: m.t.t.q313@gmail.com au kwa kupiga simu moja kwa moja (07602323733) pia unaweza kutumia mitandao ya kijamii (face book, whatsap, vaiber na telegram).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: