Mkoa wa Qaadisiyya ni moja ya vituo vya mradi wa (matibabu bila malipo) Hospitali ya rufaa Alkafeel yakusudia kuisambaza huduma hii katika mikoa mingine..

Maoni katika picha
Mradi wa (matibabu bila malipo) unao endeshwa na hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wenye lengo la kusaidia wakazi wa mijini na vijijini.

Ulianza kutekelezwa katika mkoa wa Karbala tukufu kwa kuwafanyia watu vipimo vya kiafya na kuwapatia dawa bure kutokana na maradhi yao, baada ya kumaliza hatua ya kwanza katika mkoa wa Karbala tukufu sasa wameanza hatua ya kwenda katika mikoa mingine, na sasa hivi wameweka kambi katika mkoa wa Qaadisiyya, vijiji vya Majihal mji wa Rubaish kusini mwa mkoa.

Hospitali imetuma jopo la madaktari kwa ajili ya kubaini miji inayo hitaji huduma hii.

Katika mara hii, wamesha fanyiwa uchunguzi karibu watu (500) katika mambo mbalimbali, ikiwemo; macho, ngozi na tumbo. Hii ni moja ya hatua za jaula (mzunguko) katika mkoa huu, tunatarajia kufika katika miji mingine na maeneo yenye wakazi wengi wa kipato cha chini (mafakiri) katika siku zijazo kulingana na ratiba yetu iliyo andaliwa na idara ya hospitali ya rufaa Alkafeel.

Mradi umepokelewa vizuri sana na wakazi wa miji hii, hakika walistahili kupata huduma hii.

Kumbuka kua mradi wa matibabu bila malipo ulio anza kutekelezwa katika mji wa Karbala tukufu unalenga mambo yafuatayo:

Kwanza: Kutambua mazingira ya kiafya katika kila eneo hasa maeneo yenye uchache wa vituo vya afya.

Pili: Kuelezea tiba muafaka na kuitekeleza chini ya usimamizi wa daktari bingwa.

Tatu: Kuchangia katika kupunguza matatizo ya kiafya kwa wakazi.

Nne: Kuwazoesha wakazi kupima ayfa zao na kupata ushauri wa kidaktari.

Tano: Kuondoa hali ya kuziasi hospitali na kusimamia katika kuwapa matibabu stahiki baada ya kuwapima.

Sita: Kufahamu hali halisi ya matatizo ya kiafya kimaeneo, na aina ya maradhi yanayo wasumbua, na kuyatafutia tiba stahili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: