Zimesha andaliwa mada maalumu za kozi hii na kuwekwa katika mihadhara itakayo rushwa katika (YouTube) ya mtandao maalumu wa Maadadi, kila mshiriki ataweza kusikiliza mihadhara hiyo bure.
Mada zitakazo rushwa zitahusu masomo yafuatazo:
- 1- Mada za Fiqhi.
- 2- Mada za Akhlaq.
- 3- Mada za Aqaaid.
- 4- Maelezo ya historia za maimamu (a.s).
- 5- Mihadhara kuhusu mimbari ya kihistoria na kimaudhui na namna ya uongeaji.
Kumbuka kua kozi hizi zinalenga kupunguza tatizo la wahubiri wa kike, na tunatarajia kupanua uga zaidi, hatimae kuboresha swala la majaalis (vikao) vya Husseiniyya vya kudumu, kwa namna na njia zinazo fahamika zaidi na zenye uhalisia na tukio. Pia idara ya mashindano katika Maahadi ya turathi za mitume (a.s) na masomo ya hauza kwa njia ya mtandao imeandaa zawadi ya mihadhara kumi ya mwanzo katika mashindano yatakayo fanyika mwishoni wa kozi.
Kwa maelezo zaidi au kushiriki katika kozi wasiliana nasi kwa: (07732907128).