Kitivo cha elimu za kiislamu chadhamini maonyesho ya turathi yanayo simamiwa na kituo cha turathi za Karbala

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za kitamaduni na kijamii zinazo angazia turathi za mji wa Karbala tukufu, na kuzitambulisha. Kituo cha turathi za Karbala kilicho chini ya kitengo cha maarifa za kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya maonyesho ya turathi ya aina yake, kwa kusaidiana na kitivo cha elimu za kiislamu cha chuo kikuu cha Karbala.

Maonyesho haya, ambayo ni miongoni mwa mfululizo wa maonyesho yanayo fanywa na kituo (cha turathi za Karbala) katika vyuo vikuu vya Iraq, yamehusisha machapisho mengi ya kitengo cha maarifa za kiislamu na kibinadamu yenye anuani karibu (70), miongoni mwa mausua (c.d), vitabu na majarida yanayo tolewa na kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Basra pamoja na kituo cha turathi za Hilla na Maahadi ya Qur an tukufu.

Vile vile yalihusisha picha za mnato (100) za aina mbalimbali za turathi za Karbala zenye maudhui (10) zilizopo katika mbao maridhawa, zinazo elezea maendeleo ya ujenzi wa Atabatu Husseiniyya tukufu katika awamu tofauti, pia palikua na nakala za kale pamoja na ramani ya mji wa Karbala tukufu ya zamani, na majina ya mitaa pamoja na alama muhimu za kale.

Maonyesho yalipata muitikio mkubwa kutoka kwa walimu na wanafunzi wa chuo, ambao waliona kua ni fursa bubwa kwao inayo wasaidia kufahamu turathi nyingi za mji huu ambao una mchango mkubwa katika historia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: