Ugeni wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ulihudhuria katika vikao cha vya taazia ya mashahidi waliouawa wakati wakipambana na magaidi wa Daish katika mji wa Qaadisiyya ulio ndani ya mkoa wa Najafu tukufu, ikiwa kama sehemu ya kuwaliwaza wana familia na kupongeza ushujaa walio onyesha watoto wao katika kupambana na magaidi hao waliokua wakielekea katika mji Amirul Mu-uminina Ali (a.s).
Alkafeel ilifanya mahojiano na Sayyid Adnani Mussawiy mjumbe wa kitengo cha dini, alisema kua: “Kutokana na maelekezo ya wakuu wa kisheria katika ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, tumekuja kushiriki katika vikao vya taazia ya mashahidi watukufu walio uawa katika mji wa Qaadisiyya uliopo ndani ya mkoa wa Najafu tukufu kutokana na tukio la magaidi wa kidaish walio kusudia mji huu mtukufu wenye amani kuja kufanya vitendo vya kiuoga na kigaidi kuua watu wasio na hatia baada ya kuwashinda katika uwanja wa vita, vitendo hivi vya kinyama vinaonyesha kufeli kwao na kushindwa”.
Akaendelea kusema kua: “Ugeni huu umehusisha masayyid na mashekhe watukufu pamoja na idadi kubwa ya viongozi. Vikao vya taazia vilifanyika katika eneo la soko la Sha’alaani lililopa katika mji wa Qaadisiyya, kikao cha kwanza kilihusu mashahidi wawili na kikao cha pili kilihusu mashahidi sita miongoni mwa mashahidi wa tukio hili la kigaidi, na ilitolewa zawadi ya kifedha kwa ndugu wa mashahidi, na kuwataka wawe na subira na watarajie shufaa kutoka kwao (mashahidi zao) siku ya kiama”.
Kumbuka kua; kabla ya siku mbili kundi la magaidi lilivamia kituo cha ukaguzi katika mji wa Qaadisiyya na kufanya jinai zao zilizo lenga askari wa ukaguzi na raia wema, tukio hili linaonyesha wazi kushindwa kwao katika uwanja wa vita dhidi ya jeshi la serikali na hashdi shaabiy watukufu, lakini njama yao ilifeli na waliuliwa magaidi wote.