Ugeni ulipokelewa katika ukumbi wa utawala wa Ataba tukufu na Muhandisi Jafari Saidi Jafari, aliwakaribisha kwa heshima zote na kuwaambia kua, huduma za matibabu wanazo taka kuzitoa kwa wagonywa zinatokana na ujumbe wao wa kibinadamu na ki-akhlaqi nayo ni miongoni mwa mambo aliyo sisitiza Mwenyezi Mungu na mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w).
Ujembe huu umekuja kwa ajili ya kujadiliana namna ya kuanzisha ushirikiano baina yao na hospitali ya rufaa Alkafeel na kuiongezea vitu tofauti kutokana na maombi ya idara ya hospitali.
Aliye fanikisha mawasiliano ya kufika kwa ugeni huu, Shekh Muhammad Jawaad Salaami mkuu wa kituo cha mahusiano ya kimataifa katika atabatu Abbasiyya alisema kua: “Ugeni huu ni wa madaktari bingwa katika mambo tofauti, kuna bingwa wa moyo, upasuaji, majeraha, sikio, koo, viungo na kuna bingwa wa umeme wa moyo na mengineyo, ziara ya ugeni huu imepatikana baada ya kuhudhuria kwa ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano la madaktari lililo fanywa na Chama cha kimataifa cha madaktari wa imamiyya katika mji wa Orlando Florida Marekani katika mwezi wa nane uliopita”.
Akaendelea kusema kua: “Lilifanyika kongamano pembezoni mwa kongamano hili pamoja na wajumbe wa Chama cha madaktari wa imamiyya, ndani ya ofisi yao, New Jersey na alihudhuria daktari Arshadi Qaumiy na Wajihi Ridhawiy wakuu wa Chama hicho cha kimataifa, tukakubaliana nao pamoja na madaktari wengine ambao hawakuhudhuria kongamano waje Karbala waangalie namna ya kufanya kazi pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na huu ni ujumbe wa kwanza inshallah utafatiwa ujumbe mwingine”.