Hashdi sha’abiy wawakirimu wanahabari wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na kazi nzuri wanayo fanya ya kutangaza ushujaa na ushindi wa Hashdi Sha’abiy na jeshi la serikali.

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo (vyombo vya habari ni mlango wa nusra iliyo ahidiwa) Hashdi Sha’abiy asubuhi ya Alkhamisi (05 Januari 2017 m) sawa na (06 Rabiul Thani 1438 h) walifanya hafla ya kuvikirimu vyombo vya habari za kusoma, kusikiliza na kuona, kutokana na mchango wao wa kutangaza habari za vita tukufu, na miongoni mwa vyombo hivyo ni vyombo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, Jarida la Swada Raudhataini na Idhaa ya Alkafeel ya wanawake, hali kadhalika kutokana na kazi kubwa zinazo fanywa na vyombo hivyo ya kuthibitisha ushindi wanao pata wapiganaji wetu dhidi ya madhalimu na matakfiri.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq kisha ikafuatia khutuba ya Ustadh Maitham Ataabiy msemaji wa Hashi Sha’abiy katika ofisi ya Karbala tukufu, ambaye alisema: “Kwa kupitia takrima hizi, tunatuma salamu za shukrani na upendo kwa watengenezaji wa amani na jamii ya raia wa Iraq, na tunawaambia enyi wana habari shupavu, nyie ndio mtengenezao ushindi na mna mkono mrefu katika kutengeneza maamuzi, tunabariki juhudi zenu kubwa na tunasema hakika uongozi wa Hashdi Sha’abiy unasimama pamoja na wanahabari wa Iraq daima, hakika ushindi wote unaopatikana katika uwanja wa vita, unao tengenezwa na wapiganaji wa kiiraq, Hashdi Sha’abiy au vikosi vingine vya wapiganaji, ushindi huo hauwezi kuwafikia wairaq na walimwengu kwa ujumla kama sio juhudi za wana habari, kwa kujitoa kwao muhanga na kusimamia kwao ukweli dhidi ya maadui zetu wanao ficha ushindi wetu”.

Halafu ilifuatia khutuba ya Naqaba Swahfataini tawi la Karbala tukufu iliyo wasilishwa kwa niaba na Ustadhi Maajid Khayaat, ambayo ilizungumzia kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuleta ushindi wa wapiganaji watukufu dhidi ya magaidi, na kujitolea kwao muhanga kwa ajili ya kufikisha ukweli kwa walimwengu.

Halfa ilikhitimishwa kwa kutoa zawadi kwa vyombo vyote vya habari za kusomwa, kusikilizwa na kuangaliwa ambavyo hutoa habari za kivita na vimechangia pakubwa kuleta ushindi kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abiy na jeshi la serikali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: