Kwa mara ya kwanza hapa Iraq na katika hospitali ya rufaa Alkafeel: Mgonjwa wa saratani afanyiwa upasuaji kwa kutumia mionzi..

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wa Iraq, wamefanikisha kuleta vifaa tiba vya kisasa na kimataifa pia wana madaktari bingwa wanao endana na vifaa hivyo, miongoni mwa vipaombele vya hospitali hii ni kutibu maradhi ya saratani ambayo yamekua mengi hapa Iraq.

Tumeona kuna haja ya kuto tegemea tiba za nje kwa maradhi haya hatari, uongozi wa juu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na idara ya hospitali ya Alkafeel wamefanikisha kuleta vifaa vya kisasa kabisa vya kutibu virusi vya saratani kwa kutumia mionzi, na wamefaulu kwa kufanya upasuaji wa kwanza wa saratani ya titi kwa kutumia mionzi hapa Iraq, chini ya usimamizi wa jopo la madaktari, kabla ya upasuaji huo madaktari walipitia taarifa za upasuaji wa aina hii uliofanywa huko nyuma karibu (20).

Dokta Leeth Sharafiy mmoja wa madaktari wa upasuaji aliiambia Alkafeel kua: “Kwa bahati mbaya bado saratani ni maradhi hatari sana, lakini teknolojia ya kutibu kwa kutumia mionzi inaleta matumaini mapya kwa wagonjwa wa maradhi haya mabaya, na tayali tumeanza kuitumia katika hospitali ya Alkafeel, jopo la madaktari wamefanya upasuaji wa kutumia mionzi kwa mgonjwa wa kike aliye kua anasumbuliwa na saratani ya titi, na tumemfanyia uchunguzi karibu mara (ishirini) baada ya kumfania matibabu”.

Sharafiy akaendelea kusema kua: “Hakika utumiaji wa kifaa cha mionzi kilichopo hivi sasa katika hospitali ya rufaa Alkafeel hapa Iraq, inachukuliwa kua ni hatua kubwa katika kutibu maradhi ya saratani kwa hatua ya kwanza na yapili, mgonjwa huwekewa mionzi kwa umakini mkubwa sehemu yenye maradhi kwa kiasi cha chini ya milimita mija, na huharakisha matibabu, kisha huendelea kufanyiwa uchunguzi kwa vikao vichache tofauti na awali, hali kadhalika huleta amani kwa mgonjwa”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali tembelea toghuti yetu: (www.kh.iq) au piga simu: (07602329999) au (07602344444).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: