Shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) zafanya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa jeshi shupavu la Iraq..

Maoni katika picha
Kigezo cha shule zingine za msingi na sekondari (upili) zilizopo chini ya ofisi ya malezi katika mji wa Karbala tukufu, shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimefanya gwaride la kumbukumbu ya kufikisha miaka (96) toka kuanzishwa kwa jeshi shupavu la Iraq, shule zilizo shiriki katika gwaride hilo ni: Shule ya msingi ya Ameed ya wavulana na shule ya Olevo (upili) ya Sayyid Al maau ya wavulana.

Mwalimu mkuu wa shule ya Olevo (upili) ya Sayyid Al maau ustadh Muslimu Hassan Alghaanimiy alisema kua: “Kushiriki katika kumbukumbu hii kunatokana na kuitambua taasisi hii muhimu ambayo inalinda nchi yetu, hakika shule za Abulfadhil Abbasi (a.s) zinazingatia kua ni miongoni mwa harakati za kielimu kufanya kumbukumbu za kitaifa kama hizi”.

Kuhusu kushiriki kwa shule hizi katika matembezi ya gwaride Ustadhi Yaasir Abdurazaaq mwalimu wa malezi na michezo wa shule ya Sayyid Al maau alisema kua: “Hakika walimu wa shule hizi wamefanya juhudi kubwa sana kuhakikisha wanafunzi wanafanya gwaride hili kwa nidhamu na umaridadi wa hali ya juu, hakika kushiriki kwetu katika kuadhimisha kumbu kumbu hii kunaonyesha jinsi tunavyo shikamana na jeshi la Iraq shupavu pia kufurahia ushindi wanao endelea kuupata dhidi ya magaidi wa kidaesh”.

Naye mwalimu wa malezi na michezo wa shule ya msingi Ameed ustadh Sa’ad Alaawi alisema kua: “Ushiriki wetu katika matembezi haya ya gwaride kunatokana na maelekezo ya uongozi wa juu wa malezi katika mkoa huu, shule zimekua zikishiriki katika kusherehekea kuanzishwa kwa jeshi la Iraq shupavu kwa ajili ya kukumbuka ushujaa wao na kuenzi ushindi wao katika vita dhidi ya ugaidi, hakika kumbukumbu hizi zinawajenga walimu pia kwa kulifanya jeshi la Iraq kama mfano wa kuigwa katika ushujaa na kujitolea kwao”.

Mwisho wa matembezi hayo, Atabatu Abbasiyya tukufu ilipewa zawadi ya ngao kutoka katika kitengo cha michezo cha ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala tukufu, ilipokelewa na ustadh Muslimu Hassan Alghaanimiy muwakilishi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: