Kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo sisitiza kuwasaidia wapiganaji wa serikali na wale wa Hashdi Sha’abiy na kusimama pamoja nao katika vita dhidi ya magaidi ya kidaesh kwa ajili ya kurejesha maeneo yaliyo twaliwa na magaidi hao hapa Iraq, Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma msafara wa misaada kwa wapiganaji waliopo Hamrain na milima ya Makhuul, msafara huu ni miongoni mwa misafara mingi iliyotumwa katika uwanja wa vita kwa ajili ya kuwasaidia wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abiy na bado inaendelea.
Mjumbe wa ugeni wa msafara, Shekh Haidari Al aaridhiy kutoka katika kitengo cha Dini cha Ataba tukufu alisema kua: “Msafara huu wa misaada ni miongoni mwa taratibu ilizo jiwekea Atabatu Abbasiyya tukufu katika kusaidia wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abiy kwa ajili ya kudumisha uimara wa mapambano na kusimama pamoja na majemedali hawa kimaanayiyya na kimaadda, huu ni msafara wa tano au wa sita katika maeneo haya, tumesha wahi kuja kuwaletea mavazi ya kujikinga na baridi, kipindi cha baridi kali na mvua, hakika jambo hili analihitajia zaidi mpiganaji wakati huu, tulileta mablangeti, mavazi, madawa na vyakula vya aina tofauti pamoja na zawadi za tabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaendelea kusema kua: “Msaada wetu haukuhusu kutoa vitu peke yake, bali tulitoa nasaha kwa kuwahusia kuongeza juhudi na kuwafafanulia hadhi na heshima kubwa waliyo nayo na hakika misaada hii si lolote kulingana na kujitolea kwao, tuliwakuta wanashauku kubwa na ujasiri wa hali ya juu, pamoja na ugumu wa hali ya hewa na mazingira yote kwa ujumla, lakini wana ari kubwa ya kupigana jihadi, yoto hii ni kutokana na imani waliyo nayo na mapenzi kwa nchi yao, na tuliwafikishia salamu kutoka kwa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wote wa Ataba wanawaombea nusra na ushindi”.
Aaridhiy akasisitiza kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada na inasimama pamoja na wapiganaji wa Iraq waliopo katika uwanja wa vita wa aina zote, ambao wamejitolea mali na nafsi zao kwa ajili ya kuihami Iraq na magaidi wa kidaesh, tutaendelea kusimama pamoja nao hadi kukombolewa kwa ncha ya mwisho ya aridhi ya nchi yetu kipenzi”.
Wapiganaji walitoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na juhudi kubwa wanayo fanya ya kuwapa misaada mfululizo, wakasisitiza kua wako imara, na wataendeleza ushindi hadi kukombolewa kwa aridhi yote kutoka mikononi mwa magenge ya kigaidi.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inazingatia sana upelekaji wa misaada kwa vikosi vya aina zote, vya serikali na Hashdi Sha’abiy, pamoja na kuunda vitengo vya kusaidia wakimbizi na familia za mashahidi pamoja na kufatilia majeruhi.