Kituo cha Ameed cha kimataifa cha utafiti na masomo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu chaendesha miradi ya kitafiti, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa (Mu’ujamu Ameed Alfaadhul Qur anul Kareem) ambao unalenga kufatilia maendeleo ya kihistoria ya matamshi ya Qur an tukufu, kwa mujibu wa mapokezi ya vitabu, mradi huu unatekelezwa na jopo la walimu wa vyuo vikuu vya Iraq.
Kwa ajili ya kufatilia utendaji wa kazi katika mradi huu, hufanywa makongamano ya kitafiti na mijadala ya kielimu kila baada ya muda fulani, kwa ajili ya kueleza walipo fikia na kutaja vikwazo kama vipo ili vitatuliwe, na kupata natija (matokea) inayo endana na hadhi ya kazi hii muhimu.
Kongamano la mwisho lililo simamiwa na Dokta Karim Hussein Naaswih mkuu wa mradi huu, liligusa mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni:
Kwanza: Kulipa umuhimu mkubwa swala la Mu’ujamu na kushughulishwa na jambo hilo zaidi kuliko mambo mengine.
Pili: Umuhimu wa kukamilisha mradi huu haraka, kwa muda uliopangwa ambao kwa muda wa juu ni 01/10/2017 m.
Tatu: Kujadili mapendekezo muhimu, kuhusu ukusanyaji wa mada na matatizo yanayo jitokeza katika utendaji.
Hali kadhalika yaliwasilishwa na kujadiliwa maswala ya kielimu kuhusu asili ya matamshi na mnyambuliko wake, pia likajadiliwa swala la kutumia kompyuta (tanakilishi) ambayo hurahisisha kazi, kwa kutafuta mambo ya kielimu na kuleta pamoja fikra za watafiti, palikua na majadiliano makali kuhusu swala hili.
Kiongozi mkuu wa mradi huu aliwataka washiriki waandae waraka utakao elezea mwenendo wa ukusanyaji wa mada, na utafafanuliwa namna ya kujaza maelezo katika waraka huo, kampa jukumu hilo mmoja wa walimu, na utajadiliwa katika kikao kijacho, pamoja na kuendelea kutafakari namna bora ya uandishi wa (Mu’ujamu).
Mwisho wa konkamano dokta ambaye ni kiongozi mkuu, aliwashukuru sana washiriki wa mradi huu kwa juhudi kubwa wanazo fanya za kuhakikisha wanakamilisha mradi wa Mu’ujamu.