Alitoka kwa ajili ya kupigana kuihami nchi, dini yake na maeneo matukufu, akiwa amebeba imani kama ngao na siraha yake, alijiunga na Hashdi Sha’abiy katika siku za mwanzo za kutolewa kwa fatwa ya kujilinda tukufu, alipigana katika miji mingi iliyo kua imetekwa na magaidi, alijitolea kuwawakilisha ndugu zake wanne walio kua na wake, akaahidi kupigana kwa niaba yao, aliingia vitani akiwa na ari kubwa ya kujitolea ujana wake na mustakbali wake wote, alipatwa na shambulizi baada ya miezi nane toka kuingia kwake katika uwanja wa vita, katika moja ya vijiji vya Swalahu Dini, kwa kushambuliwa yeye pamoja na wenzake na gari iliyo sheheni vilipuzi, shambulio hilo lilisababisha kupoteza macho yake na mkono wa kushoto na alibata majeraha mengine pia.
Mpiganaji Muhammad Naeem Kashkul ana miaka ishirini na nne, anatokea katika mji wa Swadr Bagdadi, alikuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ili asimame kwa fakhari kutokana na majeraha aliyo pata wakati akipambana kuhami nchi na dini yake tukufu, akiona ni utukufu kwake kupata jeraha linalo fanana na majeraha ya Maula Mwezi wa familia (a.s).
Mtandao wa Alkafeel ilimfata na kumuomba asimulie kisa cha ushujaa wake, kwa ufupi alituambia kua:
Nilijiunga na Hashdi Sha’abiy toka siku za kwanza za fatwa ya jihadi ya kujilinda tukufu, iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Hussein Sistani (d.dh) kwa ajili ya kupigana pamoja na ndugu zangu raia wa nchi hii, baada ya kukubaliwa na kupewa baraka zote na wazazi wangu (baba na mama) pamoja na ndugu zangu wanne ambao wamesha owa, nilitoka nikiwa na moyo mkubwa wa kupambana huenda naweza kuleta ushindi pamoja na ndugu zangu wapiganaji, au nipate heshima ya shahada katika kuihami dini na maeneo matukufu.
Nilipigana usiku na mchana, nikiwa na wapiganaji wenzangu kutoka kila pembe ya Iraq, na wa umri tofauti, kuna wadogo kwangu, wakubwa na wengine wazee, tuligawana risasi na kupigana kwa ushirikiano na tuliweza kukomboa sehemu kubwa, baadhi ya marafiki zangu walipata shahada na mimi nilitamani kuungana nao, lakini haikuwa riziki yangu, kumbe riziki yangu ilikua ni kupata majeraha katika jangwa la mji wa Tikriti baada ya kushambuliwa na gari lililo sheheni vilipuzi tukiwa katika mapambano usiku, nilipelekwa hospitalini na nilipo pata fahamu nilitambua kua nimepoteza kabisa macho yangu yote mawili na mkono wa kushoto.
Sikatai kua shambulio lilikua na machungu makubwa kwangu na kwa familia yangu pamoja na marafiki, lakini; kinacho nipa nguvu ni kwamba linanikumbusha majeraha ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na huu ni utukufu mkubwa kwangu, hii leo nasimama mbele yake nikiwa nimekosa baadhi ya viungo vyangu kwa ajili ya kumuhami na kuihami nchi yaku na dini yangu, natarajia nusra ipo karibu kwa wairaq wote na wapiganaji wote warejee salama majumbani mwao.