Ugeni wa wairaq wanataaluma wazuru Atabatu Abbasiyya tukufu na wakagua miradi yake halafu wasisitiza kua ziara hii itakua sababu ya kushirikiana katika miradi ijayo…

Maoni katika picha: sehemu ya matembezi
Kutokana na wito mtukufu wa Atabatu Abbasiyya, kufatia kujali kwake vipawa vya wairaki na kutaka kunufaika kutokana na fikra zao, ugeni wa wataalamu wa ki Iraq wamekuja kuizuru Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuangalia miradi yake na kushuhudia mafanikio makubwa yaliyo fikiwa na kufungua milango ya kushirikiana.

Shekh Dhiyaau Dini Zubaidiy alifatana nao katika jaula (matembezi), walitembelea Daarul Kafeel ya uchabaji na usambazaji (wa vitabu na majarida…) kisha wakatembelea mashamba ya Khairaati Abulfadhil Abbasi (a.s), halafu wakatembelea hospitali ya rufaa Alkafeel, wageni walipewa maelezo ya kina katika kila mradi walio tembelea kutoka kwa wahusika wa mradi huo, kuhusu vifaa na mambo wanayo fanya, jambo ambalo liliwavutia sana wageni hao.

Ziara ilikhitimishwa kwa kukutana na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swaafi (d.i) ambapo walibadilisha mawazo kuhusu miradi itakayo tekelezwa baadae ambayo manufaa yake yatakua kwa wote Inshallah.

Dokta Zaiduna Khalaf Saaidiy rais wa tume ya wataalamu wa ki Iraq aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na wito mtukufu wa muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swaaafi kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuja kuitembelea Ataba na miradi yake, ndio tumekuja sisi wajumbe wa tume ya wataalamu wa ki Iraq na tumetembelea baadhi ya miradi ya mfano, pamoja na uchache wa muda wetu lakini tumeweza kutembelea miradi kadhaa na maeneo mbalimbali, na tumekhitimisha ziara yetu kwa kukutana na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambaye ametutosheleza na alikua mkarimu sana kwetu katika maombi yetu yote, naye ni mbora wa watu walio sikia sauti yetu ambayo ilikua haisikilizwi na serikali.

Akaendelea kusema kua: “Hakika bila upendeleo, katika ziara yetu ya kutembelea miradi tumeona, miradi hii inamanufaa kwa wote, na tumekuta uwezo mkubwa sana katika miradi hiyo, mradi wa hospitani, uchapaji na mingineo na yote inahudumia jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: