Mkoa wa Qaadisiyya ni moja ya mikoa ya Iraq yenye makumbusho mengi, kuna malalo ya mtume Shuaibu (a.s) na malalo ya watoto wa maimamu na wajukuu zao (a.s), na miongoni mwake ni malalo ya Sayyid Muhammad bun Hamza bun Abdullahi bun Abbasi bun Hassan bun Abdullahi bun Abbasi bun Ali bun Abii Twalib (a.s) aliye pewa laqabu ya (Ariis), malalo yake yapo katika kitongoji cha Afki ndani ya mkoa tajwa, makumbusho (mazaru) haya yalisahauliwa na hayakujengwa kwa miaka mingi, jengo lililopo hivi sasa ni la zamani na lipo katika hali ya kienyeji mno.
Kutokana na ratiba ya kujenga makumbusho (mazaru) yote ya kishia hapa Iraq, limewekwa jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa makumbusho hii tukufu, baada ya kuandaliwa kwa ramani na michoro ya ujenzi na kitengo cha wahandisi kwa ajili ya kuanza utekelezaji, jambo hili limetia furaha katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s), ugeni uliyo wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu wenye ratiba hii nzuri ya kujenga makumbusho matukufu miongoni mwake makumbusho haya ya Sayyid Muhammad Ariis.
Katibu mkuu wa makumbusho ya kishia shekh Sataar Jizaaniy katika khutuba yake alisema kua: “Hakika kuweka jiwe la msingi katika makumbusho haya matukufu, ni miongoni mwa mipango ya uongozi mkuu ya kujenga makumbusho yote matukufu, pamoja na ukata wa mali unao ikumba Iraq, huu hautakua mradi wa mwisho, bali huu ni mwanzo, tutaendelea na miradi ya ujenzi katika makumbusho yote na kutatua matatizo yao kutokana na utukufu wake na heshima ziliyo nayo makumbusho hayo kihistoria na kijamii kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na mazuwaru”.
Katika hafla hii alihudhuria pia mshauri wa katibu mkuu wa makumbusho (mazaru) na wakuu wa vitengo pamoja na wawakilishi wa Ataba tukufu hali kadhalika mashekhe wa makabila na wasomi wa kisekula na viongozi wa mji wa Afki pamoja na mazuwaru watukufu.