Hospitali ya Alkafeel yaanza kutumia kifaa cha Gamma Camera katika vipimo vyake, yasisitiza kua ni kifaa cha kisasa kabisa katika upimaji wa magonjwa..

Maoni katika picha: mmoja wa wana kliniki
Idara ya Twibu Nnawawi katika hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutumia kifaa cha (Gamma Camera) ambacho ni kifaa cha kisasa kabisa katika ulimwengu wa tiba kimataifa, hutumika katika kutambua maradhi ya moyo na virusi vya saratani katika sehemu mbali mbali za muili wa mwanadamu.

Mtumishi wa kitengo cha Twibu Nnawawi Daktari Muhammad Sa’aduni Shammaau katika hospitali ya rufaa Alkafeel alisema kua: “Kifaa hiki ni moja ya vifaa tiba vilivyopo katika hospitali ya ruaa Alkafeel, ni kifaa bora zaidi katika upimaji wa maradhi mbali mbali, hubainisha hali ya maradhi na kina uwezo mkubwa wa kutambua tatizo lolote katika kiungo cha mwanadamu, na hubaini maradhi yakiwa katika hatua ya kwanza kabisa jambo ambalo hurahisisha katika matibabu yake”.

Shammaau aliendelea kusema kua: “Hakika Gamma Camera ni kipimo muhimu kwa maradhi ya saratani ya figo na saratani ya matiti pamoja na aina zingine za saratani, pia hupima maradhi mengine yasiyo kua ya saratani, vilevile kinauwezo wa kupima ini na kuangalia mirija ya kwenye ini pamoja na mambo mengine”.

Akaendelea kusema kua: “Tofauti kati ya Gamma Camera na kifaa cha MRI, ni upimaji wa kimaumbile.

Kifaa cha MRI huonyesha umbo la kiungo na ukubwa au unene wa sehemu husika, huku kifaa cha Gamma Camera huonyesha sehemu husika ya kiungo pamoja na kufafanua umbo la kiungo na kipimo kinabainisha shida ya mgonjwa na sio mgonjwa abaineshe shida yake”.

Akafafanua kua: “Kifaa hiki kinaendeshwa na jopo la wataalamu wakubwa walio bobea katika mambo haya, na wamesha fanyiwa vipimo wagonjwa wengi na wote walipata majibu chanya”.

Kwa maelezo zaidi na kufahamu huduma zinazo tolewa na hospitali tembelea toghuti ya hospitali: (www.kh.iq) au piga simu (07602329999) au (07602344444).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: