Tarehe 10 Rabiul Thani ulimwengu uliangaziwa na nuru kwa kuzaliwa imam Hassan Askariy (a.s)..

Maoni katika picha
Nyumba ya mtume mtukufu na wafuasi wao na kila anaye wapenda walipata furaha tarehe kumi Rabiul Thani mwaka 232 h. katika mji wa Madina kwa kuzaliwa nuru miongoni mwa nuru za mtume mtukufu, na kupokelewa na baba yake imam Ali Haadi (a.s) kwa furaha na bashasha, kwa sababu ni muendelezo wa kizazi cha mtume na warithi wa elimu ya manabii na mawasii, akafanya haraka kuandaa sherehe za mazazi kama alivyo kua anafanya mtume (saww) walipo zaliwa Hassan na Hussein (a.s), akaadhini katika sikio la kulia la mtoto na akakimu katika sikio la kushoto na siku ya saba, akanyoa nywele za mtoto na akatoa fedha kwa uzani wa nywele hizo na akachinja beberu wa hakika kisha akampa jina la Hassan, na akampa jina la kunia ya (Abuu Muhammad), akamlea malezi mema ya mitume na akamfundisha adabu na hekima, akakua chini ya mapenzi na usimamizi wa Mwenyezi Mungu kama mtume alivyo mlea imam Ali (a.s), ukadhihiri utukufu na elimu ya imam Hassan Askariy toka akiwa mdogo.

Imam Askariy ni imam wa kumi na moja katika maimam wa nyumba ya mtume (s.a). jina lake kamili ni: Hassan bun Ali bun Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abaatwalib (a.s).

Mama yake anaitwa (Judaith) wengine wanasema alikua anaitwa (Saliil) alikua mwanamke mwema mnyenyekevu na mchamungu, yatosha katika kuelezea wasifu wake kauli ya imam Haadi (a.s): (Saliil ametakasika na mapungufu na amesitirika na uchafu).

Imam Hassan Zakiyyu alishika madaraka ya uimam baada ya kufariki baba yake Haadi (a.s) mwaka wa 254 h. akiwa na umri wa miaka 22, uimamu wake ulidumu kwa miaka sita na miezi kadhaa, alishika madaraka ya uimam mwishoni mwa ufalme wa Mu’utaz Al abbaasiy aliye kaa mwezi mmoja akafa kisha akashika ufalme Muhtada, naye alidumu miezi kumi na moja kisha mfalme Mu’utamadi bun Mtawakil, imam Hassan Askariy (a.s) alifariki katika zama za huyu mfalume wa mwisho. Imam Hassan (a.s) aliishi na baba yake miaka ishirini na tatu.

Amekua mashuhuri zaidi kwa laqabu ya Askariy, kutokana na sehemu ilipo nyumba ya baba yake ilikua ikiitwa (Askari) mji huu ulikua miongoni mwa miji fakiri, pia ulifanywa kua ni makazi ya askari, miongoni mwa mambo muhimu kwa imam Hassan Askariy (a.s), aliandaa mazingira ya ghaiba ndogo na kubwa kwa wafuasi wake.

Imam Hassan Askariy (a.s) alikua mwalimu wa wanazuoni, kigezo chema cha wapenda haki, kiongozi wa wana siasa hakika alikua ni mtu wa kupigiwa mfano katika kila nyanja, hata wapinzani wake walikiri utukufu wake.

Miongoni mwa sifa za imam Hassan Askariy (a.s) alikua mweusi mwenye kimo kizuri na uso mzuri, alikua na haiba kubwa, aliheshimiwa na kila mtu kutokana na utukufu wake, upole wake, zuhudi na wingi wa ibada zake, ukarimu wake, pete yake ilikua imeandikwa (Ametakasika yule ambaye usimamizi wa mbingu na aridhi ni wake) au (Mimi kwa Allah ni shahidi) au (Allahu shahiid) nahirizi yake ilikua ni: (Ewe marejeo yangu wakati wa shida zangu, ewe unaye nisamehe ninapo jikurubisha, ewe liwazo langu wakati wa upweke wangu, nilinde kwa jicho lako lisilo lala, na unitosheleze kwa rehema zako zisizo isha).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: