Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu waizuru familia ya Shahidi Raaidu Khalidi Majidi aliyekua katika kikosi cha washika bunduki cha jeshi la umoja, wasisitiza kua kila wanacho toa kwa ajili mashahidi ni kidogo mno kutokana na hadhi yao..

Sehemu ya ziara
Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), ugeni wa Ataba tukufu umeenda kuitembelea na kuipa taazia familia ya Shahidi Raaidu Khalidi Majidi Yaasi aliye kua katika kikosi cha washika bunduki cha jeshi la umoja, aliye pata shahada hivi karibuni kwa ajili ya kuilinda aridhi ya Iraq na raia wake dhidi ya magenge ya magaidi katika vita vinavyo endelea vyenye kauli mbiu isemayo (Tunakuja ewe Nainawa).

Familia ya shahid iliupokea ugeni huu kwa furaha na walithamini sana kutembelewa huko, wakajifakhari kwa shahada ya mtoto wao pamoja na kwamba ni pigo kumkosa lakini walionesha kua shahada hiyo ni kwa ajili ya kuihami aridhi ya nchi yao.

Mkuu wa msafara Shekh Aadil ambaye ni wakili msaidizi wa rais wa mambo ya kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Huyu shahid alikua na nafasi maalumu katika nyoyo za viongozi na watumishi wa jeshi la umoja, alipambika na tabia nzuri na uhodari, alikua tayali kujidhuru kwa ajili ya kutekeleza wajibu wake, ziara hii ni miongoni mwa ratiba za Atabatu Abbasiyya tukufu, kuwasiliana na familia tunazo ziangalia kwa jicho la ufahari na utukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Tumeikirimu familia hii kutokana na alicho kifanya mtoto wao mwema kwa ajili ya kulinda aridhi ya nchi hii tukufu, ambayo imeloana kwa damu za shahidi pamoja na wengine walio mtangulia, hakika kila tutakacho toa kwa ajili yao hakilingani hata chembe na namna walivyo jitolea, tunasema malipo ni kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, bila shaka wako peponi inshallah”.

Kumbuka kua Shahidi Raaidu Khalidi Majidi Yaasi (r.a) amezaliwa (1985 m) na alikua mkazi wa Karbala tukufu, alikuamwanafunzi wa chuo cha uhandisi mwaka wa tatu, ameshiriki katika mapigano mengi na mwisho wake ilikua ni vita vya Mosul aliko pata utukufu wa shahada 31/12/2016m, akiwa anapigana kwa ujasiri huku ameinua kichwa chake kwa ajili ya kulinda aridhi ya nchi yake na kujitolea kila anacho weza kukitoa kwa ajili ya nchi yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: