Kitengo cha usimamizi wa kihandisi chaendelea na matengenezo katika paa la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Kutokana na ratiba ya usimamizi iliyo wekwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo husu kukagua maeneo yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia ndani hadi nje ya haram kwa kufata muda na sehemu, jambo hili limefanya kazi ziwepo kila siku bila kusimama, miongoni mwa kazi zinazo endelea sasa hivi ni matengenezo ya paa la haram tukufu hadi kwenye paa lililo ndani ya mradi wa upanuzi wa Ataba na paa la uzio.

Kazi inayo fanyika sasa hivi kwa mujibu wa watumishi ni; kuinua sehemu zinazo takiwa kuinuliwa kutokana na mradi wa upanuzi wa Ataba na kusafisha sehemu zinazo takiwa kurekebishwa.

Baada ya kumaliza kazi hizo vikawekwa vipawa mbele vya kazi, miongoni mwake ni kubadilisha mabomba ya maji ya mvua, kwa kuweka mabomba mapya yenye ubora mkubwa tofauti na yale yakwanza, na kwa uwekaji mpya vile vile, unao endana na paa la sasa, mabomba hayo yametengenezwa na kukusanywa katika chumba chenye ukubwa wa mita (325).

Hali kadhalika tumeinua nyaya za umeme na zingine tumebadilisha na kuzifunga kwa namna nyingine pia tumeweka marumaru sehemu ya chini ya nguzo ya saa sehemu yenye ukubwa wa mita (16).

Matengenezo haya yalihusisha pia uwekaji wa msingi katika sehemu za ndani ya haram tukufu kwa ukubwa wa mita (500) ikiwa pamoja na kufunika mabomba ya sistim ya utiaji baridi na kubadilisha yaliyo haribika na kurepea yenye kasoro.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: