Kwa mara ya kwanza hapa Iraq: Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji yaingiza kifaa cha uchapaji wa nakala za kale kwa kutumia (Facsimile)..

Maoni katika picha
Miongoni mwa hatua za maendeleo zinazo lenga kuingiza kila aina ya fani mpya katika uchapishaji na umuhimu wa kunufaika na teknolojia za kisasa, Darul Kafeel inayo husika na uchapaji na usambazaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeingiza kifaa cha kisasa kabisa katika uchapaji wa nakala za kale, kifaa hicho kina uwezo wa kuchapa vitabu vya kale katika umbo lake lile lile la asili, kifaa hiki (Facsimile) ni miongoni mwa teknolojia mpya inayo shuhudiwa kwa mara ya kwanza hapa Iraq, na kinasaidia kuhifadhi nakala halisi yenye hati ya asili, tofauti na kuchapa nakala mpya yenye muonekano tofauti.

Mkuu wa kitengo cha machapisho, Ustadhi Farasi Ibrahimiy aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hatua hii iliyofikiwa na kituo cha uchapishaji ni kwa ajili ya kuhifadhi hati za asili na hasa zile ambazo ni nadra, na kutoa fursa kwa watafiti na wahakiki kuzama katika hizi turathi tajiri, na kilicho tushajihisha kufanya hili ni kwa sababu Atabatu Abbasiyya tukufu inahazina kubwa ya nakala za kale na inawataalamu rasmi wa sekta hiyo, hivyo tulianza kwa kukifanyia kazi kitabu kale cha Mukhtasar wa vikao vya ma alawi (Muktasar Maraasimul Alawiyya) cha muhakiki Hilliy (676 h) ambacho kilitolewa na kituo cha turathi za Hilla”.

Akaendelea kusema kua: “Tulijitahidi kutoa nakala mpya inayo fanana sana na nakala ya zamani kwa asilimia (%90) kuanzia hati na umbo la kitabu kwa ujumla hadi baadhi ya vitu vidogo vidogo vilivyomo ndani ya kitabu hicho, tulirepea baadhi ya maandishi ya sura katika nakala ya zamani kwa kutumia program maalumu ya tanakilishi (computer), na yalikua sawa na maandishi ya asili kwa kiasi kikubwa sana pia mfanano wa rangi, uchapaji, aina ya karatasi na mistari pamoja na mfanano wa karatasi katika kila ukurasa, kuanzia kava hadi kava (mwanzo hadi mwisho) kadhalika tumetengeneza kava linalo fanana sana na kava la nakala ya asili, ili kumfanya msomaji ahisi anasoma ile ile nakala ya asili kuanzia kava hadi kava, pamoja na kusherehesha baadhi ya maneno au herufi zilizo kua zimeharibika au kufutika, kazi hii inahitaji umakini mkubwa na muda mwingi ili kutoa kitabu chenye sifa za kielimu na ubora wa maandishi na muonekano, na tumetoa nakala mbili, moja ya asili na nakala iliyo hakikiwa na kurekebishwa”.

Kumbuka kua kuanzishwa kwa mradi wa uchapishaji wa vitabu na usambazaji (Darul Kafeel) ni miongoni mwa plani za Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kujenga uwezo wa kujitegemea, na kuhakikisha tunamiliki vifaa vya kuchapisha vitabu, majarida na nyaraka zingine, ilituchangie katika kuongeza utamaduni wa kusoma kwa namna ambayo itamnufaisha muandishi na msambazaji kwa kuongeza uzuri wa chapisho na kupunguza gharama, tuna vifaa vya uchapishaji vya kisasa kabisa kimataifa, ilikujibu haja ya Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi zingine za usambazaji wa vitabu na majarida ili kuwapatia mali bora na yenye umakini wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: