Kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha katika Maahadi ya Qur an chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya nadwa ya kielimu kwa kushirikiana na kitivo cha maarifa ya kiislamu cha chuo kikuu cha Karbala, ya kutambulisha mwenendo wa vizito viwili na mashindano ya muandishi bora kuhusu Qur an tukufu katika mwenendo wa vizito viwili.
Maelezo yaliyo tolewa na mkuu wa kituo shekh Dhiyaau Dini Zubaidi yalipata muitikio makubwa kutoka kwa walimu wa chuo, watafiti na wanafunzi, pia nadwa iligubikwa na mijadala ya kielimu, Shekh Zubaidi alielezea mafanikio ya kituo cha maarifa ya Qur an.
Pembezoni mwa nadwa hiyo, kilifanyika kikao kilicho muhusisha mkuu wa kitivo cha maarifa ya kiislamu na rais wa kitengo cha maarifa ya Qur an na rais wa kitengo cha Fiqhi pamoja na mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha kilicho chini ya Atabatu Abbasia tukufu pamoja wa wageni walio ongozana nao, walizungumzia kuhusu kufungua milango ya kusaidiana katika mambo yanayo husu Qur an tukufu, kama sehemu ya kutoa huduma ya mambo yanayo husu Qur an ndani ya vyuo vikuu vya Iraq na miongoni mwake chuo kikuu cha Karbala, mwishoni mwa kikao hicho; mkuu wa kitivo cha maarifa ya kiislamu katika chuo kikuu cha Karbala, dokta Haashim Naasir Kaabiy aliomba wapewe vitabu vingi vinavyo chapishwa na kituo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha ili wavitumie katika selibasi ya masomo katika ngazi tofaiti, pia ombi kama hili limesha wahi kutolewa na chuo kikuu cha Basra na kile cha Dhiqaar.
Kumbuka kua kituo kimesha kamilisha miradi kadhaa ya Qur an, miongoni mwake ni: kuchapisha msahafu wa kwanza kuchapishwa hapa Iraq tena kwa juhudi za wairaq wenyewe katika hatua zote, pia mradi wa kalamu inayo tamka Qur an tukufu na tafsiri yake na mradi wa mausua (mtiririko) wa visomo vya Qur an, na tayali yamesha chapishwa majuzuu mengi hadi hivi sasa, vile vile wametoa kitabu cha muongozo wa mwalimu na muongozo wa mwanafunzi, na mengineyo mengi.