Kitengo cha usafirishaji (magari) ya Atabatu Abbasiyya tukufu chafanya juhudi kubwa ya kusaidia vitengo vya Ataba na kuhudumia watu wanaokuja kufanya ziara..

Maoni katika picha
Kitengo cha usafirishaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya juhudi kubwa katika kusaidia vitengo vingine vya Ataba kutekeleza majukumu yao kwa kuwapa usafiri wa dharura kwa ajili ya kutekeleza kazi zao, pamoja na huduma ya kuwabeba bure watu wanao kuja kufanya ziara, ikiwemo kusambaza maji masafi katika mawaakibu (makundi ya wahudumu) za Husseiniyya hususan katika ziara za mamilioni ya watu zinazo shuhudiwa katika Ataba za Karbala tukufu.

Ili kufahamu zaidi kuhusu kazi za kitengo hicho mtandao wa Alkafeel ulikutana na rais wa kitengo Ustadh Abduljawaad Kaadhimu Abbasi ambaye alisema kua: “Kitengo hiki kina mamlaka ya kutumia vyombo vyote vya usafiri vikubwa na vidogo vya Atabatu Abbasiyyya tukufu, pamoja na kutoa huduma ya usafiri wa bure kwa watu wanao kuja kufanya ziara, kwa ajili ya kuwarahisishia kutimiza ibada zao, na katika ziara za mamilioni ya watu hua tunawachukua kutoka maeneo zinako ishia gari za nje na kuwaleta hadi karibu na Ataba tukufu na kuwarudisha katika maeneo ya kupandia gari kwa wale wano rudi, pia hutoa usafiri kwa vitengo vingine vya Ataba kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza kati zao ikiwemo magari makubwa, madogo na yale ya kusambaza maji masafi, bila kusahau magari ya wagonjwa, yanayo saidia kuwapeleka hospitalini wakati wowote linapo tokea tatizo la ugonjwa kwa mtu yeyote, jumla ya magari yote ni (216) ya aina mbali mbali na ukubwa tofauti”.

Akaendelea kusema kua: “Kitengo hiki kimegawa kazi katika idara tofauti, na kila idara inahusika na jukumu lake maalumu, idara hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Idara ya mafundi (Gerage): Inajukumu la kukagua magari ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pia ina idara ndogo ndoga nyingi miongoni mwake ni idara ya mapokezi, ambayo hupangilia utokaji na uingiaji wa gari, na kuna idara ya stoo, ambayo huhifadhi vifaa vya magari ya Ataba vya aina mbalimbali.
  2. Idara ya usimamizi: Husimamia utendaji wa magari, pia huteua aina ya gari linalo faa kwenda kutekeleza jukumu lililo hitaji gari miongoni mwa vitengo vya Ataba, na huandika matumizi ya gari hilo katika daftari maalumu linazo sajili ufanyaji kazi wa magari wa kila siku, katika daftari hilo huandikwa, muda wa kutoka kwa kila gari na muda wa kurudi, aina ya gari na namba yake na jina la dereva, na wanufaika pia huandikwa idadi za kilometa, kabla ya kutoka na baada ya kurudi.
  3. Idara ya mali: Nayo inahusika na mambo ya kiofisi, kama vile kufatilia mahudhurio ya wafanya kazi, na kufatilia ujazaji wa vitabu vya kitengo hiki, na inajukumu la kufatilia mambo yote yanayo husu mali (pesa) ndani ya kitengo hiki.
  4. Idara ya kubeba mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara): Nayo inahusika na kubeba mazuwaru bure, kuwatoa na kuwapeleka sehemu mbali mbali”.

Kuhusu watumishi wa kitengo hiki alisema: “Kitengo hiki kina watumishi (430) wamegawanyika katika idara nilizo zitaja, muda wao wa kazi hutofautiana kutokana na kutofautiana kwa idara, baadhi ya idara watumishi wao huingia asubuhi na jioni tu, na nyingine huingia asubuhi, jioni na usiku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: