Maahadi Kafeel kwa wenye mahitaji maalumu ni hatua nzuri ya kuwa andaa watu wenye ulemavu katika mji wa Karbala tukufu..

Mmoja wa watahiniwa wa maahadi
Pamoja na matatizo yanayo zikumba taasisi za kielimu na kimalezi, bado hazitilii umuhimu au haziwajali baadhi ya makundi ya watu katika jamii, hasa watu wenye mahitaji maalumu, kama vile watoto wenye ulemavu, jambo ambalo limepelekea Atabatu Abbasiyya kubeba jukumu hili la kuwafundisha na kuwajengea misingi ya kuishi na jamii kidini na kuchunga afya zao, ndipo ikafunguliwa Maahadi Kafeel kwa watu wenye mahitaji maalumu katika barabara ya Hussein (a.s) kwa ajili ya kulea watoto hawa bure.

Kwa ajili ya kufahamu zaidi kuhusu (Maahadi Kafeel kwa watu wenye mahitaji maalumu) iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu mtandao wa Alkafeel uliitembelea na kufanya mahojiano pamoja na Ustadhat Sarah Hassan Hafaar mkuu wa maahadi na alikua na haya ya kusema: “Wenye mahitaji maalumu; tunalenga watoto wenye ulemavu mwepesi (wanao weza kusomesheka), anaweza kua ni mlemavu wa akili (tahira) au wenye matatizo ya kujitenga na ukimya wa kupitiliza, wengine wanamatatizo ya kuongea au ya kusikia.. watoto hawa hupimwa na madaktari katika vituo vya afya hapa Karbala ili kuthibitisha matatizo yao kisha huletwa katika maahadi (kituo) yetu kutokana na kutokuwepo kwa kituo kingine kama hiki katika mji wa Karbala tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Tunapokea watoto wa jinsia zote mbili,watoto wa kike kuanzia umri wa miaka (6-15) na wavulana miaka (6-12) baada ya kupimwa na kuthibitishiwa na daktari kua wanaweza kusomesheka, na hupewa majaribio chini ya usimamizi wa dokta wake kwa muda maalumu hapa ndani ya maahadi, pia hujadiliwa uwezo wake wakupokea masomo pamoja na mahitaji yake ya lazima ambayo maahadi itatakiwa kumtimizia kisha ndio anakubaliwa kujiunga na maahadi”.

Kuhusu masomo wanayo someshwa alisema kua: “Selibasi ya masomo ina viwango tofauti, mwanafunzi hupitia hatua sita za masomo, kuna mada hufundishwa kwa kutumia picha zilizo geuzwa na zinaweza kuunganishwa kwa uwepesi, somo la lugha linahusisha pia vipange vya picha na herufu na somo la hesabu vile vile linahusisha picha na namba pamoja na hesabu nyepesi nyepesi, kuna somo la mambo yanayo izunguka jamii, kuna masomo ya Ahklaqi na masomo ya kiislamu, tunawafundisha Qur an tukufu sura fupi fupi na hadithi za mtume, pia tuna masomo ya michezo, na tunawafundisha kazi za mikono zitakazo wafaa katika maisha yao zipo kazi za aina tofauti katika kumbi tofauti, kila mmoja anasoma kazi anayo penda, pia tuna mbao za kisasa kabisa za kufundishia, vitu hivi vinatusaidia kua na maendeleo mazuri, hadi hivi sasa maahadi ina wanafunzi (70) wakati ilianza na wanafunzi ishirini mwaka (2009m), kila baada ya mwaka mwanafunzi hupewa jaribio la kupima maendeleo yake na kujua kama anaweza kujiunga na shule za kawaida au lhawezi”.

Akaongeza kua: “Tunafanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana, pia hua tunatumia magari ya Atabatu Abbasiyya katika kubeba wanafunzi wetu, na hua tunafanya safari za kwenda kutembelea sehemu mabali mbali za kihistoria na kimazingira (kuburudika) ndani na nje ya Karbala tukufu, maahadi imepata maendeleo makubwa katika kurekebisha kiwango cha akili kwa wanafunzi wetu”.

Kuhusu huduma wanazo pewa mtoto mwenye ulemavu Hafaar alisema kua: “Mtoto mwenye matatizo ya akili (tahira) yeye mwenyewe hajitambui wala hawezi kutambua matatizo ya mtu mwingine, katika maahadi tuna malezi ya jumla na tunatoa huduma kwa wote kwa kumchanganya mtoto na wenzake, hua tunatumia mbinu zinazo faa za kuwashajihisha na kuwafanya wajitambue”.

Akamalizia kwa kusema: “Itaendelea kazi kua rahisi katika Maahadi Kafeel ya kutoa huduma ya kuwalea na kuwasomesha bure watu wenye ulemavu bila kua na mshindani, pindi serikali inapo shindwa kutekeleza jambo ni jukumu la taasisi za kiraia kujenga jamii yao kadri ya uwezo wao, itaendelea kazi hii tukufu iliyo asisiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kujenga heshima kwa Ataba na watumishi wake bila shaka matunda ya kazi hii yataonekana hivi karibuni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: