Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi ya Baharul Uluum Al khairiyya waendelea na maandalizi ya kongamano la pili litakalo husu uhuishaji wa mimbari ya Husseiniyya..

Maoni katika picha
Katika kukamilisha maandalizi ya kongamano lililo anza kufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Baharul Uluum Al khairiyya chini ya kauli mbiu isemayo (hauza za kielimu ni sehemu bora ya uhuishaji) kamati ya maandalizi yaendelea na vikao vyake vya kujadili na kupanga namna ya uendeshaji wa kongamano la pili litakalo fanyika tarehe kumi na sita na kumi na saba ya mwezi wa tatu mwaka huu (2017 m), chini ya kauli mbiu isemayo (Kongamano la kimataifa kuhusu uhuishaji wa mimbari ya Husseiniyya) kutokana na nafasi kubwa zilizo nazo majaalisi za imam Hussein (a.s) katika kufundisha tabia za Ahlulbait (a.s) na kuutambulisha uislamu sahihi katika jamii, unaoshambuliwa kila kona, kifikra, kiteknolojia na katika mitandao ya kijamii na uharaka wa kufikisha ujumbe bila kizuizi kupitia mitandao hiyo.. jambo hili limeonyesha haja kubwa kwa khatibu wa mimbari ya imam Hussein apambike kwa upole, hekima, uadilifu na kuvumiliana, pia ajiepushe na kila aina ya ubaguzi na chuki jambo ambalo laweza kuupasua umma wa kiislamu, ahakikishe anawaunganisha waislamu wote waishi kwa amani pamoja na wanadamu waote kwa ujumla.

Shekh Muhsin Alkhuzaai mjumbe wa kamati ya maandalizi alisema kua: “Kuzungumzia kuhusu mimbari ya imam Hussein (a.s) yenye uwelewa na mafuhumu pana na nafasi ya pekee katika kufundisha itikadi sahihi na kuelekeza umma katika mwenendo wa imam Hussein (a.s) wa kudumu ni maelezo yenye nyanja nyingi, na yote yanatokana na Qur an tukufu pamoja na sunna takasifu, unapokua umuhimu wa mimbari hii ni kuleta islahi (maelewano) katika jamii, hakika huo ndio ujumbe mkubwa wa Ashuraa, maelewana hayawezi kupatikana bila kubainisha vitu vinavyo weza kuchangia katika kuleta maelewano, hivyo jukumu sio la khatibu peke yake anaye ongea katika mimbari, inatakiwa kila mmtu atekeleze wajibu wake katika kufikia lengo la kuleta maelewano”.

Akaendelea kusema kua: “kutokana na ratiba ya maandalizi, siku ya kwanza ambayo Itakua na hafla ya ufunguzi, itakua ni siku ya Alkhamisi (16/03/2017m) sawa na (16 Jamadal Aakhar 1438h) katika mji mtukufu wa Najafu ndani ya majengo ya taasisi ya Baharul Uluum Al khairiyya, kutakua na mada za kitafiti asubuhi na jioni, siku ya pili ambayo itakua Ijumaa (17/03/2017m) sawa na (17 Jamadal Aakhar 1438h) kongamano litahamia katika mji wa Karbala ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu zitaendelea kutolewa mada za kitafiti kisha itafanyika hafla ya ufungaji wa kongamano”.

Unaweza kuwasiliana na kamati ya maandalizi kwa njia zifatazo:

Simu: 009647802222543

Email: info@h-najaf.iq

Toghuti: www.h-najaf.iq

Face book: https//www.facebook.com/hauza.najaf
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: