Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada la kumi na tatu. imefanya kikao kilicho husisha wakuu wote wa vitengo vya kongamano hilo siku ya Juma Mosi asubuhi (15 Rabiul Aakhar 1538h) sawa na (14 Januari 2017m) katika ukumbi wa Sayyid Auswiyaau ndani ya Atabatu Huseeiniyya tukufu, kwa ajili ya kujadili yaliyo fikiwa katika vikao vilinyo pita na yaliyo tekelezwa, pamoja na kupokea maoni yanayo lenga uboreshaji wa kongamano hili kupitia uzoefu wa makongamano yaliyo pita, na wasimamizi wa kongamano hili ni Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Naibu katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya ambaye ni mjumbe katika kamati ya maandalizi Sayyid Afdhal Shaamiy aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Leo tumefanya kikao cha kamati ya maandalizi pamoja na viongozi wote wa vitengo vya kongamano kwa ajili ya kubainisha majukumu ya kila kitengo ili waanze utekelezaji wa majukumu yao, kwa sababu miaka ya nyuma iliwahi kutokea kuingiliana katika utekelezaji wa majukumu kwa baadhi ya vitengo, mwaka huu tumebainisha majukumu ya kila kitengo kwa uwazi zaidi, ili kila kitengo kifahamu majukumu yake kuanzia sasa, na tumekitaka kila kitengo kifanye kikao kila wiki cha kujadili maandalizi yao na wakabidhi ripoti zao katika kamati kuu ya maandalizi, wataandika vikwazo na tutaangalia namna ya kuvitatua, pia watatoa mapendekezo yao ambayo tutayajadili kwa pamoja, kwani kongamano hili ni muhimu sana kwetu, kama tulivyo kubaliana kuanza kuandaa mabango ya matangazo sasa hivi ili tuweze kuyajadili, na zoezi hili liweze kukamilika mapema inshallah.
Naibu rais wa kitengo cha utamaduni na habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye ni mjumbe katika kamati ya maandalizi ya kongamano hili, Sayyd Aqeel Abdulhussein Al yaasiriy alisema kua: “Kikao hiki ni miongoni mwa vikao vinavyo fanywa na kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada lakini umuhimu wa kikao hiki, kimeweza kuhudhuriwa na wakuu wote wa vitengo vya kongamano pamoja na baadhi ya wajumbe wao na tumeainisha kanuni za msingi za kila kitengo na zimejadiliwa na kutolewa ufafanuzi na wajumbe wa kamati kuu ya maandalizi”.
Tunapenda kusema kua; kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada huandaliwa na kuendeshwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kila mwaka kuanzia tarehe tatu Shabani, kwa kuzingatia tarehe ya kuzaliwa kwa imam Huseein, Abulfadhil Abbasi na imam Sajaad (a.s).