Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada ya kumi na tatu yatangaza masharti ya mada zitakazo shindaniwa katika kongamano..

Sehemu ya kikao
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada ya kumi na tatu Shekh Ammaar Hilali ametangaza mada zitakazo shindaniwa, na masharti ya kushiriki katika mashindano ya kitafiti yatakayo fanyika sambamba na kongamano la mwaka huu chini ya kauli mbiu isemayo: (Imam Hussein (as) ni kisima kirefu na chemchem endelevu) nazo ni kama zifuatazo:

Mada za Akhlaq:

 • 1- Imam Hussein (as) ni kigezo cha mwanadamu mkamilifu na mfano wa pekee.
 • 2- Athari ya kutafakari katika kuutambua uokovu wa nafsi.. Huru - mfano.
 • 3- Mafhumu ya kufanya wema hatakama unakudhuru.. Abbasi (as) - mfano.

Mada za Fiqhi:

 • 1- Visababishi vya jihadi kati ya Twafu na Hashdi.. Fatwa ya Marjaa – mfano.
 • 2- Ugaidi na misingi yake ya kifiqhi kati ya Twafu na vikundi vya kitakfir.
 • 3- Heshima ya damu, mali na cheo kati ya (siku ya) Ashura na leo.

Mada za kisheria na kisiasa:

 • 1- Haki za binadamu kati ya mafundisho ya imam Hussein (as) na mtazao wa kimataifa.
 • 2- Mjadala wa haki na wajibu katika mafuhumu ya twafu.
 • 3- Utekelezaji wa haki kati ya raia na kiongozi.
 • 4- Athari ya kutumia muda wa baadae katika kurekebisha jamii kwa kutumia ujumbe wa haki, bi Zainabu (as) – mfano.
 • 5- Habari za kivita na athari yake katika kuleta ushindi kutokana na mtazamo wa vizito viwili.

Kuhusu masharti ya mashindano, Alisema kua: Kamati ya maandalizi imeweka kanuni na masharti ya tafiti zitakazo wasilishwa katika mashindano kama ifuatavyo:

 • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kusambazwa na watu wengine kabla yako.
 • 2- Utafiti uandikwe kwa kuchunga kanuni za kielimu.
 • 3- Utafiti usiwe chini ya kurasa (15) na zisizidi (30),

uandikwe kwa hati ya (Arabic simplified) yenye ukubwa wa maandishi saizi (14) na uwekwe katika (CD).

 • 4- Utafiti usizidi maneno (300) na uambatanishe na mukhtasari wake.
 • 5- Kila utafiti uambatanishwe wasifu wa muandishi, utafiti wowote utakao kosa wasifu wa muandishi hautazingatiwa.
 • 6- Utafiti utumwe pamoja na wasifu wa muandishi na picha yake pamoja na namba ya simu na email, kwa njia ya email au unaweza kupelekwa moja kwa moja katika kitengo cha mambo ya Maarifa ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu au unaweza kupeleka katika taasisi ya Ulumu Nahju Balagha ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu, mwisho wa kupokea tafiti hizo ni (1 Rajabu 1438h).

Zawadi za washindi ni:

Mshindi wa kwanza: (1,000,000) milioni moja dinari za Iraq.

Mshindi wa pili: (750,000) laki saba na elufu hamsini dinari za Iraq.

Mshindi wa tatu: (500,000) laki tono dinari za Iraq.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:

rabee@alkafeel.net au almaaref@alkafeel.net au inahj.org@gmail.com au kwa namba zifuatazo:

(07723757532) na (07728243600) na (07815016633).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: