Kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidh wa Qur an tukufu kilicho chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya vikao vya kila wiki vya usomaji wa Qur an tukufu, wanashiriki wasomaji wa mji wa Karbala tukufu pamoja na miji mingine, kisomo hiki hufanywa kila usiku wa Ijumaa baada ya Magharib na Ishaa katika Sardabu ya Imam Hassan (as) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kusimamiwa na wasomaji wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), husikilizwa kisomo cha mshiriki kisha hutolewa maoni ya kitaalamu na maelekezo kutoka kwa wasikilizaji, yanayo saidia katika kuboresha usomaji. Siku ya kwanza imepata mahudhurio makubwa kutoka kwa wasomaji wa Karbala na miji mingine, kikao hiki kiliongozwa na mkuu wa kuandaa wasomaji na mahafidh wa Qur an Sayyid Hussein Halou, aliwasikiliza wasomaji na kutoa baadhi ya maelekezo kwao.
Washiriki walizishukuru sana Ataba tukufu kwa kuandaa vikao hivi na kusema kua; vina waimarisha na kuwaboresha zaidi katika usomaji wa Qur an tukufu.
Kumbuka kua; kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidh wa Qur an tukufu mara nyingi huendesha kozi za hukumu za usomaji na mas ala ya sauti na naghma, pia hufanya miradi ya Qur an kwa lengo la kuandaa wasomaji bora zaidi.