Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji yajitolea kuchapa vipeperushi vya kufundishia Hashdi Sha’abiy na mkufunzi atoa shukrani kwa jambo hilo..

Maoni katika picha
Kama sehemu ya kuendelea kuwasaidia wapiganaji wa Hashdi Sha’abiy, Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamejitolea kuchapisha vipeperushi vya kufundishia Hashdi Sha’abiy bure, vitakavyo tumika katika kufundisha wapiganaji na maelekezo ya utumiaji wa siraha pamoja na ramani na mengineyo.

Ustadh Kaadhim Jabri Jaasim mkuu wa kitengo cha ukufunzi katika Hashdi Sha’abiy alisema kua: “Hakika tunashukuru sana msaada huu unaofanywa na Darul Kafeel kwa kuchapa vipeperushi vya kufundishia, jambo huli litaongeza ari ya wapiganaji wa Hashdi Sha’abiy”.

Kumbuka kua A tabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada na kusimama pamoja na wapiganaji wa vikosi vyote, kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo sisitiza jambo hilo, na misaada inahusu nyanja nyingi, kuna inayo tolewa katika uwanja wa vita, na mingine ya kutembelea familia za mashahidi na majeruhi, na hili linalo fanywa na kitengo cha uchapishaji cha Darul Kafeel ni moja katika misaada pia.

Kwa mawasiliano zaidi na Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji waweza kutembelea ofisi zetu zilizopo katika mji wa Karbala tukufu, barabara ya Ibrahimiyya, au piga simu namba zifuatazo:

009647823950890

009647706733834

009647602335433
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: