Hospitali ya rufaa Alkafeel ayasisitiza kua ratiba yake ya uokozi wa kitabibu imepunguza udhia wa kusafirishwa wagonjwa nje na ina matokeo mazuri..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu daktari Haidari Bahadeliy amesisitiza kua; Ratiba ya uokozi wa kitabibu inayo endeshwa kwa kushirikiana na wizara ya afya, imepata mafanikio makubwa katika kufanya upasuaji ambao hauwezi kufanywa na hospitali zingine hapa Iraq, na kuokoa pesa ambazo zingetumika kwa ajili ya kuwapeleka wagonjwa nje pamoja na wasindikizaji wao.

Akaendelea kusema kua: “Tumeweka mpango kazi wa kutekeleza makubaliano ya kuleta madaktari bingwa wa kimataifa kadri itakavyo hitajika au inavyo hitajika, tutalifanya hili kwa nguvu zetu zote kwa ajili ya kufanikisha huu ushirikiano kati ya wizara ya afya na hospitali ya rufaa Alkafeel, ili iwe ya kimataifa sawa na zile ambazo wairaq walikua wanazifata nje ya nchi kwa ajili ya matibabu”.

Kiongozi wa idara ya uokozi wa kitibabu Ustadh Abbasi Faadhil Hamaadiy alisema kua: “Hadi sasa tumesha pokea wagonjwa (418) kutoka wizara ya afya wenye maradhi tofauti, wagonjwa wa moyo, macho na wa aina mbali mbali za upasuaji”.

Akasema: “Tumesha wafanyia uchunguzi wagonjwa wa moyo (119), jopo la madaktari bingwa wa kigeni limewafanyia upasuaji wa moyo wagonjwa kumi na wote kazi imeenda vizuri na wengine watafanyiwa baadae, na wagonjwa (40) wa macho tumewafanyia upandikizaji katika macho yao, matibabu ya aina hii yamefanyika kwa mara ya kwanza hapa Iraq, jumla tumewafanyia uchunguzi wa macho wagonjwa (223) ambao walikua na matatizo tofauti”.

Kuhusu upasuaji, Hamaadiy alisema: “Kitengo chetu cha upasuaji kimefanya upasuaji (21) wa aina tofauti, tuliwafanyia uchunguzi wagonjwa (52) na tumewafanyia upasuaji wagonjwa (14) wakiwemo walio fanyiwa kwa kutumia kifaa cha (Ilizarov) ambacho hakikuwepo hapa Iraq siku za nyuma”.

Kumbuka kua ratiba ya uokozi wa kitibabu inayo simamiwa na wizara ya afya ya Iraq, na kumaliza tatizo la kuwatuma wagonjwa wenye matatizo magumu nje ya nchi na badala yake kuwaleta katika hospitali ya rufaa Alkafeel, kutokana na ubora wa huduma pamoja na kuwepo kwa vifaa tiba vya kisasa na madaktari bingwa wenye uzoefu mkubwa na mafanikio katika kazi zao.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali tembelea toghuti yetu: www.kh.iq au piga simu: (07602344444) au (07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: