Kitengo cha mali chategemea baraka za mwenye ukarimu Abulfadhil Abbari (a.s)..

Maoni katika picha
Kitengo cha mali ni miongoni mwa vitengo hai katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kina jukumu la kulea na kutekeleza maombi ya fedha za kuendeshea miradi au za matumizi katika vitengo vingine, ikiwemo mishahara ya watumishi. Kwa ajili ya ufanisi katika kazi yao na kutunza mali za Atabatu Abbasiyya tukufu wanafuata utaratibu na kanuni za kimataifa katika utunzaji wa mahesabu.

Kitengo hiki kiliundwa sambamba na vitengo vingine baada ya kuanguka kwa utawala uliopita (utawala wa Sadam) nacho kinahusika na maswala yote ya mali za Ataba tukufu zinazo patikana kutokana na pato la ndani au la nje.

Ili kufahamu zaidi kuhusu kitengo hiki, tuliongea na rais wa kitengo ustadh Qais Dahaan alikua na haya ya kusema: “Kitengo hiki kina jukumu la kupokea na kutoa mali zote zinazo ingia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kutoka katika vyanzo vyake vya mapato au kwa wahisani ambao hukabidhi katika kitengo cha zawadi na nadhiri kisha kitengo hicho hukadidhi kwetu mali hizo kwa utaratibu ulio wekwa, pia kitengo cha mali ndicho hupokea fedha zote zinazo tengwa kutoka katika wakfu ya shia kama mishahara ya watumishi, kadhalika pesa zinazo toka katika miradi ya kiuchumi”.

Kuhusu mgawanyo wa kazi kiofisi alisema kua: “Kitengo cha mali kina idara (12) kila idara inawajibika katika majukumu yake maalumu, nazo ni:

 • 1- Idara ya mishahara: Huandaa malipo ya mishahara kwa watumishi pamoja na kuangalia mabadiliko ya malipo kwa kila mtumishi.
 • 2- Idara ya hazina: Hubaini kiasi kilichopo katika hazina baada ya kutoa matumizi ya Ataba tukufu katika kila mwezi.
 • 3- Idara ya miradi ya kiuchumi: Inajukumu la kufanya mahesabu ya miradi yote ya kiuchumi iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu
 • 4- Idara ya mali zisizo hamishika: Inanya kazi chini ya ofisi ya kutunza kumbu kumbu na pamoja na ofisi ya hazina.
 • 5- Idara ya matumizi: Inahusika na manunuzi ya vifaa vinavyo tumika kila siku au mara kwa mara katika vitengo vya Ataba.
 • 6- Idara ya mahesabu ya hazina: Inahusika na kutoa na kuingiza mali zilizopo katika Ataba tukufu kwa kushirikiana na idara ya hazina.
 • 7- Idara ya bima: Inahusika na maswala yote ya bima za miradi ya Ataba tukufu.
 • 8- Idara ya pensheni: Inahusika na maswala yote yanayo husu penshen za watumishi (kiinua mgongo) na hufanya kazi zake kwa kushirikiana na idara ya mishahara.
 • 9- Idara ya mahesabu ya miradi ya kihandisi: Inajukumu la kukagua mali zinazo tumika katika miradi yote inayo tekelezwa na Ataba tukufu.
 • 10- Idara ya wahasibu: Inajukumu la kukagua mahesabu na kupangilia nyaraka za malipo katika vitengo tofauti vya Ataba na kutunza kumbu kumbu katika daftari maalumu.
 • 11- Idara ya watumishi: Inahusika na kufatilia mambo yote ya kiofisi kwa wafanya kazi, kama vile ujaza madaftari na kukagua mahudhurio na ruhusa za wafanya kazi.
 • 12- Kituo cha kibiashara: Nacho ni kituo chenye mahitaji yote muhimu ya wakina mama na mahitaji ya nyumbani na wauzaji wake ni wanawake.

Baada ya kuangalia kazi na juhudi kubwa zinazo fanywa na ndugu zetu katika kitengo cha mali cha Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeona uhalisia uliopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ukizingatia kua ni taasisi inayo kua, na inafanya juhudi ya kuhakikisha kua inatoa huduma bora kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: