Kamati kuu inayo simamia mashindano ya Mahdawiyya kubwa ya tano, yatangaza na kuonyesha zawadi kubwa katika mikoa mitatu..

Maoni katika picha
Kamati kuu inayo simamia mashindano ya Mahdawiyya kubwa ya tano imetangaza na kuonyesha zawadi kubwa ambayo ni (Gari aina ya Sonata 2017) katika mikoa mitatu, ambayo ni:

  • 1- Karbala tukufu, imewekwa katika kituo cha bidhaa za Alkafeel namba (1) barabara ya imam Huseein (a.s).
  • 2- Najafu tukufu, imewekwa katika kituo cha bidhaa za Alkafeel namba (10) barabara ya Jaamia mkabala na shule za Bankiya.
  • 3- Basra, imewekwa katika jengo la (Time scowir) katika eneo la milimani.

Yamewekwa mabango maalumu ya matangazo kuhusu mashindano haya, pamoja na ufafanuzi wa kanuni na masharti ya mashindano, ambayo jumla ya zawadi zitakazo tolewa ni (Gari kumi za Sonata 2017 na nafasi 100 za umra), kamati ya maandalizi imesema kua; wamefanya hivi kwa ajili ya kutoa nafasi kwa washiriki wengi zaidi, kwa lengo la kueneza tamaduni na elimu ya imam Mahdi (a.f).

Kumbuka kua mashindano haya yalianza kutangazwa toka mwezi wa nane 2016m, pale walipo ambiwa wataalamu wa kitengo cha habari na utamaduni kufanya msafara wa matangazo ya kuwataka watu wajitokeze katika kushiriki mashindano haya yanayo lenga kueneza tamaduni kuhusu imam Mahadi (a.f) kwa kujaza dodoso lenye maswali kuhusu imam Mahadi (a.f).

Tambua kua; vituo vya mauzo vilichaguliwa kwa umakini mkubwa, nayo ni sehemu za kihistoria (mazaru) tukufu huko mikoani, na vituo vya mauzo vilivyo chini ya Ataba pamoja na vituo vya Nuru Alkafeel vilivyopo katika mikoa hiyo, kwa mujibu wa jopo la wasimamizi, mashindano haya yamefurahiwa sana na watu tofauti, watu wengi wameona kua ni njia sahihi kuelekea katika mwenendo mzuri, yanalenga kujenga maelewano chanya kati ya Ataba tukufu na jamii ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: