Kwa ajili ya kusaidia uzalishaji wa kitaifa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na ugeni ulio fatana naye watembelea shirika la Itihaadi lenye viwanda vya chakula katika mkoa wa Baabil..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) pamoja na katibu mkuu Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t) wakiwa na ujumbe ulio ongozana nao, asubuhi ya siku ya Alkhamisi (20 Rabiul Thani 1438h) sawa na (19 Januari 2017m) walitembelea shirika la Itihaadi lenye viwanda vya chakula katika mji wa Shomaliy ndani ya mkoa wa Baabil.. ziara hii ni sehemu ya kuunga mkono uzalishaji wa chakula kitaifa, na kujenga mawasiliano na ushirikiano kati ya viwanda hivi na Ataba tukufu.

Naibu katibu mkuu alikua ni miongoni mwa ugeni ulio tembelea viwanda hivi na alikua na haya ya kusema: “Huu ni ugeni wa kiwango cha juu kabisa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na katibu mkuu Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t) na ugeni ulio fuatana nao, kwa ajili ya kuja kutembelea shirika la Itihaadi lenye kiwanda cha sukari na zaituni katika mji wa Shomaliy ndani ya mkoa wa Baabil, tumefanya ziara hii kwa ajili ya kuunga mkono uzalishaji unaofanywa na viwanda hivi”.

Akaendelea kusema kua: “Huu ni mradi wa kitaifa; ukizingatia kua hiki ni kiwanda kikubwa cha chakula hapa Iraq, na sio kwamba kinauwezo wa kulisha Iraq peke yake, bali kinaweza kulisha hadi nje ya nchi, pia tunajenga maelewano na mahusiano katika mambo mbali mbali ili kulitumikia taifa hili inshallah”.

Hakika tumeona maendeleo makubwa katika kiwanda na ya kisasa, njia zinazo tumika katika usimamizi wa kimitambo na mpangilio bora wa kiofisi pamoja na mambo mengine mengi, maendeleo makubwa hayo pia tumeyashuhudia katika kiwanda cha zaituni, hii ni fahari kwetu kuwepo kwa viwanda kama hivi.

Naye rais wa kamati ya uongozi katika shirika la Itihaadi linalo miliki viwanda vya chakula ustadh Muhammad Hussein Naamaaniy alisema kua: “Tunaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na ugeni alio ongozana nao kwa kufanya ziara hii tukufu, ziara hii inamaana kubwa sana kwetu, ina tutia moyo wa kuongeza juhudi katika uzalishaji wa viwanda vyetu ili tuweze kulisha taifa, hasa baada ya kupata wito kutoka kwa muheshimiwa unao tutaka tuboreshe uzalishaji kwa ajili ya kutosheleza soko la ndani, ukizingatia kua tunategemea kuanzisha mradi wa mashine za usagaji, na tunatarajia kutoa unga bora kabisa inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: