Maahadi ya Qur an tukufu yaendesha kozi ya kujenga uwezo wa walimu wa Qur an katika jiji la London kupitia tawi lake la huko..

Sehemu ya kozi
Tangu kuasisiwa kwa tawi la kitengo cha Qur an tukufu katika jiji la London, imekua ni miongoni mwa majukumu yake makuu kufundisha lugha ya kiarabu na Qur an tukufu kwa kuandaa ratiba zinazo endana na viwango vya walengwa.

Kozi hii imepewa anuani isemayo: (Njia za ufundishaji maarifa ya Qur an tukufu kutoka katika kitabu cha muongozo wa mwalimu), na imesimamiwa na kitengo cha maarifa ya Qur an na kuifasiri na kuichapisha –kilicho chini ya Maahadi tajwa- ilihudhuriwa na mkuu wa kituo Shekh Dhiyaau Dini Zubaidi, ambaye alisema kua: “Katika kozi hii iliyo fanyika ndani ya ukumbi wa Noor hapa London, washiriki wamesomeshwa umuhimu wa maarifa ya Qur an tukufu katika mwenendo wa vizito viwili (Qur an tukufu na kizazi cha mtume) na njia za ufundishaji wake kutokana na kitabu cha muongpzo wa mwalimu, ambacho ni miongoni mwa machapisho ya kituo hiki, na kimepasishwa na wataalamu wengi pia kinategemewa na baadhi ya vyuo vikuu vya Iraq katika kufundishia hatua za kwanza.

Akaendelea kusema kua: “Selebasi ya kozi hii imelenga masomo ya awali katika kufahamu njia zinazo saidia kuifahamu Qur an na sherehe zake pamoja na masomo ya vitendo, na mwisho wa kozi vitatolea vyeti vya ushiriki vinavyo toka Maahadi ya Qur an tukufu katika Atabatu Abbasiyya”.

Kumbuka kua lengo la kufunguliwa kwa tawi la Maahadi ya Qur an katika jiji la London ni kutoa huduma za kielimu kwa kufundisha masomo yanayo husu Qur an tukufu kwa kufata mwenendo wa maimamu wa nyumba ya mtume (a.s) na liwe ni daraja la kuunganisha tawi hili na Maahadi zingine za Qur an, zilizopo katika mikoa mbali mbali ya Iraq, na uwe ni mwanzo mwema wa kuendelea kufungua vutuo vingine nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: