Hospitali ya Alkafeel yaokoa uhai wa mpiganaji wa hashdi sha’abi, na wana ndugu wasifu juhudi za madaktari na wauguzi..

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweza kuokoa uhai wa mpiganaji wa hashdi sha’abi aliye pata majeraha mabaya sana yaliyo karibia kuchukua uhai wake katika mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na juhudi za madaktari walio simamia matibabu yake, uhai wake umeokoka.

Kiongozi wa jopo la madaktari walio simamia matibabu yake, doktari Mu-ayyadi Naqibu alisema kua: “Hali ya mpiganaji Haidari Swalehe ilikua sawa na hali za wapiganaji wengi wanao letwa katika hospitali ya Alkafeel, wakati wa mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul akiwa katika mtaa wa Salaam ailishambuliwa na bomu moja kwa moja lililo sababisha kupoteza mguu na kuvuja damu nyingi sana, alipoteza karibu chupa(20) za damu”.

Akaendelea kusema kua: “Alipo fikishwa hapa hospitali na kumfanyia uchunguzi, alifanyiwa upasuaji (operation) tatu, baada ya juhudi kubwa na ujasiri wa mgonjwa tulifanikisha kuzuia uvujaji wa damu uliokaribia kuchukua uhai wake, kisha aliongezewa karibu chupa (25) za damu, ili kufidia damu aliyo poteza, na aliwekwa katika chumba chenye uangalizi maalumu (cha wagonjwa mahutihuti) hadi alipo pata nafuu”.

Ndugu wa majeruhi walitoa shukrani nyingi kwa uongozi wa hospitali na madaktari waliosimamia matimabu kutokana na juhudi kubwa waliyo shuhudia kwa madaktari hao, iliyo wapa imani ya kuendelea kwa uhai wa mgonjwa wao baada ya kutoweka kwa imani hiyo, lakini kwa baraka ya Mwenyezi Mungu na juhudi za madaktari mgonjwa amepona.

Kumbuka kua; hospitali ya rufaa Alkafeel ilitangaza –kupitia kiongozi wake daktari Haidari Bahadeli- kua: “Hakika uongozi wa juu wa Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kufunguliwa kwa hospitali hii iliweka vipawa mbele vyake, miongoni mwa vipawa mbele hivyo ni kuwasaidia kimatibabu na kiuangalizi majemedari wa fatwa ya kujilinda tukufu, walio jitolea damu zao kwa ajili ya kulinda heshima ya nchi hii tukufu na kuhakikisha kua aridhi yake hainajisiwi na magaidi wa kidaesh, kwa hiyo imesimama imara kupokea majeruhi kwa kuwasiliana na madaktari wa hashdi aha’abi waliopo katika viwanja vya vita au kwa kutoa huduma za moja kwa moja kupitia zana zilizo wekwa na idara ya hospitali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: