Umwagiliaji wa vioo wa moja kwa moja katika mradi wa upanuzi wa paa la uwanja wa haram tukufu..

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutumia njia ya kumwagilia maji katika mahema ya vioo iliyopo juu ya paa la uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambako kuna maeneo yametengenezwa rasmi kwa ajili ya shughuli za usafi, hizi ni shughuli za awali, baada ya kukamilika utengenezaji wa njia za maji kutakua na mradi maalumu wa kusafisha kwa kumwagia maji.

Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimesha teua watu watakao tekeleza jukumu hilo baada ya kuwapatia kozi maalumu kutoka katika shirika lenye uzoefu na kazi hii, haya mabomba ya kumwagilia ni sehemu ya mpangilio mkubwa unao husisha vyumba vya ulinzi vinavyo fungamana na chumba kikuu cha ulinzi.

Vifaa vya kumwagilia vimeunganishwa na vifaa vya udhibiti maji ambavyo vipo otumatik vinafungulia maji kwa kiasi kinacho hitajika, na vimefungwa katika pande nne za paa la uwanja wa haram tukufu katika usawa wa nguzo nne zinazo beba paa, kila moja ina nguvu za kiasi cha (mb 75) inamwaga maji kwa nguvu kutokea katika mabanda ya vioo yaliyopo juu ya paa na yanasambazwa kupitia kifaa kilichopo juu ya banda kilicho onganishwa na mabomba, kifaa cha kusambaza maji sio haya tu, kinasambaza hadi maji ya mvua pia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: