Jarida la Riyahaini ni miongoni mwa majarida bora kabisa, nalo ni jarida la kwanza kutolewa na idara ya watoto na makuzi iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kuwajenga wtoto katika aqida (imani) ya kiislamu, kupitia visa na picha zenye ufanisi wa hali ya juu, na kwa kuzingatia kua mafundisho kwa watoto ni sawa na matofali ya kwanza yanayo wekwa katika msingi wa jengo, hivyo ndio wakati ambao hujengwa msingi wa fikra za kila mwanadamu, kulikua na umuhimu mkubwa wa kupatikana kwa mafundisho bora yatakayo muelekeza mtoto katika utukufu, hususan zama hizi ambazo tunapambana na tamaduni mbaya zinazo tishia kuwaharibu watoto, mabadiliko halisi katika kila jamii huanza katika tabaka la watoto, tukitaka kubadilisha jamii yatupasa tuanze na watoto hakika wao wana uwezo mkubwa wa kusoma na kubadilika.
Rais wa wahariri wa jarida hili Ustadh Ali Badri aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tulitoa jarida la Riyahaini kutokana na mahitaji ya jamii hasa kwa watoto wenye umri mdogo, Atabatu Abbasiyya tukufu imejitahidi kufikisha sauti ya Ahlulbait (a.s) kwa makundi yote ya wairaq hadi kundi la watoto, muelekeo wetu katika mwaka wa (2009) ulikua ni kutoa jarida kwa ajili ya kundi hili muhimu, kama anavyo sema imam Ali (a.s) “ni sawa na aridhi tupu mbegu yeyote itakayo pandwa itamea”.
Akaendelea kusema kua: “Jarida hili hutolewa kila mwezi na lina kurasa arubaini, lina milango mingi isiyo badilika na mingine hubadilika katika kila toleo, kama vile milango ya visa vifupi vifupi na picha, huandikwa ndani ya jarida hili mafundisho ya tabia mepesi mepesi kwa kuzindatia umri wa walengwa ambao ni miaka (5 - 12), pia lina mafundisho mengi ya kitamaduni na kielimu, ikiwepo mambo yanayo husiana na maumbile ya dunia kama vile miti na wanyama pamoja na mambo mengine mengi yanayo saidia kufungua akili ya mtoto, na limeitwa Riyahaini, kwa kutaka baraka za wajukuu wa mtume (s.a.w.w) ambao huitwa (Rehani wawili) Hassan na Hussein (a.s) pia kila mtoto ni Rehani kwa mama yake na baba yake”.
Akaendelea kusema kua: “Leo hii jarida limepata muitikio mkubwa hapa Iraq, kuna watu wengi wanao shiriki katika uandishi na uchoraji kwa kiwango cha miji ya kiarabu, nina amini kua jarida la Riyahaini lina nafasi kubwa katika ulimwengu wa tamaduni za watoto na lina marafiki wazuri katika ulimwengu wa kiarabu, kuna watu wengi sana wanao lifatilia katika nchi mbali mbali, kwani tumeweka vionjo mbali mbali vya fani za kufundishia watoto, na tumechocheo mapenzi yao katika jarida hili kwa kuweka shindano linalo wataka watoto washiriki, na kuna muitikio mkubwa wa watoto kushiriki shindano hilo, tuna amini kwa matashi ya Mwenyezi Mungu baada ya miaka michahe tutashuhudia kizazi kipya kitakacho kua na uwelewa mkubwa katika jamii”.
Akaendelea kusema kua: “Kama mnavyo fahamu Riyahaini ni mradi kamili, sio kwamba ni jarida pekeyake, hapana! Kuna machapisho mengi yanayo fungamana na jarida hilo, vikiwemo vitabu vya elimu mbali mbali, ikiwemo elimu kuhusu Qur an, mashairi na qaswida, na kuna machapisho yanayo husu hashdi sha’abi kwa ajili ya kuwajenga watoto wawe na moyo wa kujitelea katika kulinda nchi, pamoja na mambo mengine ambayo huchaguliwa kutoka katika idhaa ya Riyahaini ambapo huhusisha qaswida na maigizo ambayo hutolewa na kikosi cha wafatiliaji wa kipindi cha watoto”.
Kuhusu usambazaji wa jarida hili Badri alisema kua: “ Jarida huwekwa katika vituo maalumu vya mauzo ya bidhaa za Ataba tukufu pamoja na sehemu mahasuhi za machapisho ya vitabu vya watoto, pia husambazwa katika shule za watoto kwa kuviuza kwa bei ya chini kabisa”.
Kumbuka kua idara ya watoto ina machapisho mengi sana ambayo yanayo lenga watoto kwa ajili ya kujenga kizazi salama chenye tamaduni na mtazamo wa Ahlulbait (a.s).
Kuona machapisho hayo tembelea mtandao wetu ufuatao: https://alkafeel.net/publications/view.php?id=15