Mradi wa kituo cha kuegeshea magari wa Alkafeel waendelea vizuri..

Maoni katika picha
Mradi wa maegesho ya magari wa Alkafeel unaendelea vizuri, hadi sasa umekamilika karibia asilimia themanini (%80), asilimia hizo zinagawika katika sehemu zote tano zinazo jumuisha mradi huu, hii ni asilimia inayo kubalika kwa mujibu wa maelezo ya Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nao ndio wasimamizi wakuu wa utekelezaji wa mradi huu.

Akaongeza kusema kua: “Mradi wa maegesho ya magari wa Alkafeel unachukuliwa kua ni miongoni mwa miradi mikubwa na muhimu katika miradi inayo fanywa na Atabatu Abbasiya tukufu, mradi gani wa namna hii unaweza kupata matatizo ya ucheleweshaji, kama ikitokea hivyo itakua ni nje ya uwezo wetu na nje ya uwezo wa idara ya shirika linalo tekeleza mradi –nayo ni mashirika mawili, la Aridhi tukufu na shirika na uzalishaji la Alkafeel- ikitokea kua hawajafanya juhudi ya kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa na kwa ufanisi ulio tarajiwa. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, malengo ya mradi huu yako wazi, umelenga mkoa wa Najafu tukufu upande wa Karbala takatifu na kinyume chake, mradi unavutia kwa ubunifu mzuri na utekelezwaji wake makini”.

Akaendelea kusema kua: “Mradi umekamilika kwa asilimia kubwa katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na sehemu za kumbi.

Sehemu (A): Sehemu za maegesho ya magari na vyoo, pamoja na kumbi/vyumba vya watumishi, kama vile vyumba vya walinzi (vyumba vya kutolea tahadhari za umeme na moto pamoja na vitu vingine) sehemu hii ina hatua tatu na zimekamilika kwa asilimia (%75) takriban, pia sehemu hii inajumuisha kituo cha mafuta kilifunguliwa kwa majaribio katika ziara ya arubainiyya iliyo pita, kina uwezo wa kutunza lita milioni moja na elufu sabini na tatu za mafuta (diesel na petrol) kuna matenki (29) kila moja lina uwezo wa kutunza lita elufu thelathini na saba, pia sehemu ya kituo chamafuta kimezungukwa na vyumba vya ofisi za wasimamizi wa kati hiyo, na kuna kitengo maalumu za kulinda magari.

Sehemu (B): Sehemu kuegesha magari madogo imekamilika kwa asilimia zaidi ya (%90).

Sehemu (C): Nayo ni sehemu ya kuegesha magari makubwa, imekamilika kwa asilimia (%85).

Sehemu (D): Nayo ni sehemu ya kuhifadhia magari (madogo na makubwa) nayo imekamilika kwa zaidi ya asilimia (%75).

Sehemu (E): Nayo ni sehemu ya jengo lenye ghorofa mbili la kuegeshea magari, ghorofa la kwanza ni kwa ajili ya maegesho ya magari makubwa na inaukubwa wa kuingia magari (102) na ghorofa la pili ni kwa ajili ya magari madogo na inaukubwa wa kuingia magari (225) na imekamilika kwa asilimia (%70).

Kituo hiki kimewekwa mitambo ya umeme na mahodhi ya maji ya mvua pamoja na mitambo ya kutoa tahadhari ya moto, na kimezungushiwa uzio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: