Utoaji wa mialiko: Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu yajiandaa kutoa zawadi kwa wanafunzi walio ongoza katika vyuo vikuu vya Iraq..

Maoni katika picha
Walimu wa vyuo vikuu na maahadi za hapa Iraq wameanza kujiandaa na zeozi la kutoa zawadi kwa wanafunzi walio shika nafasi za kwanza katika vyuo, zoezi ambalo huandaliwa na kuendeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu, chini ya mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo, wameanza kutoa mialiko kwa watu maalumu na wanafunzi, inafanyika kwa mwaka wa tano mfululizo.

Ustadh Maahir Khaalid mtumishi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu alisema kua: “Kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshika nafasi za kwanza kutoka katika kila chuo kunasaidia kujenga ari mpya katika nafsi njema za hawa watu muhimu, pia kunaongeza moyo wa kujituma kwa wanafunzi wote, tamasha hili litafanyika mwezi ujao likifungamana na kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), kutokana na mialiko tuliyo toa tunatarajia hafla hiyo itakua na muitikio mkubwa kutoka katika vyuo vyote vya Iraq kaskazini hadi kusini, na jambo la pekee katika hafla ya mwaka huu ni kuhudhuliwa na walimu wazoefu (wakongwe) katika ufundishaji kutoka katika kila chuo kikuu”.

Maraisi na wakuu wa vitivo walio pata mualiko nao walikua na haya ya kusema: “Hakika ni jambo zuri sana linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya la kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo walio shika nafasi za kwanza, sisi kwa upande wetu tunatoa shukrani za dhati kwa waandalizi wa hafla hiyo, tuna muomba Mwenyezi Mungu ajalie hafla hizi ziendelee kwa ajili ya kusaidia kukuza vipawa vya elimu, na kutolewa kwa msaada wa kimanawiyya na kimadda kwa wanafunzi wetu, pia hafla hii inasaidia kujenga uhusiano kati ya vyuo vikuu na kuanza kwa ukurasa mpya, hakika hili ni jambo zuri sana; kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu katika aridhi hii tukufu, katika uwenyeji wa mwenye ukarimu kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi walio faulu, bila kujali mielekeo yao, bali wanakusanywa pamoja kutokana na elimu zao na si vinginevyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: