Atabatu Husseiniyya yaweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji wa Karbala na Atabatu Abbasiyya yashiriki katika hafla hiyo na kuibariki..

Sehemu ya uwekaji wa jiwe la msingi
Atabatu Husseiniyya tukufu asubuhi ya leo (22 Rabiul Thani 1438h) sawa na (23 Januari 2017m) wameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimatafa utakao jengwa kati kati ya mji wa Nafafu na Karbal, sehemu yenye umbali wa kilometa (30) kutoka katikati ya mji wa Karbala tukufu, mradi huu utatekelezwa na shirika la Copper chase la wingereza pamoja na kikundi cha uzalishaji cha Rida wakishirikiana na shirika la Khairatu Sibtwaini lililo chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu.

Hatua hii itausaidia sana mji wa Karbala pamoja na watu wanao kuja kufanya ziara, hakika imefikiwa baada ya juhudi kubwa, awamu ya kwanza ya ujenzi inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi (18).

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi iliyo fanyika katika eneo la tukio, ilihudhuriwa na kiongozi mkuu kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu na katibu wake mkuu pamoja na idadi kubwa wa viongozi wa Ataba hiyo, vile vile palikua na ugeni mkubwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ukiongozwa na katibu mkuu muhandisi Muhammad Ashiqar (d.i) aliye fatana na idadi kubwa wa viongozi na wakuu wa vitengo vya Ataba, pia palikua na idadi kubwa ya viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Karbala na spika wa bunge la mkoa pamoja na baadhi ya watu muhimu katika mji wakiwemo viongozi wa kikabila, hafla ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur an tukufu kisha ilisomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi, halafu ikafuatia khutuba ya kiongozi mkuu kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu, muheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika ni muhimu kufanya mradi huu kwa ajili ya watu wanao kuja kufanya ziara na kwa heshima ya mji wa Karbala mtukufu, ukizingatia ujio wa mamilioni ya watu kila mwaka. Hakika tusinge fikia katika utekelezaji wa mradi huu kama sio utukufu wa bwana wa mashahidi imam Abuu Abdillahi Hussein (a.s) na juhudi pamoja na ikhlasi iliyo fanywa na pande nyingi kwa kuanzia na wizara ya uchukuzi, hakika wamefanya juhudi kubwa mno kuhakikisha mradi huu unaanza kutekelezwa, bila kumsahau mkuu wa mkoa wa Karbala pamoja na bunge lake na kamati ya uchumi ya kitaifa, hali kadhalika shirika la Khairatu Sibtwaini lililo chini ya Atabatu Husseiniyya (a.s), shukrani zetu za kufanikisha kwa mradi huu zinawaendea wote, tuna watakia wote heri na baraka kwa juhudi zao”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika miradi mikubwa inaweza kutekelezwa pamoja na matatizo tunayo pitia hapa Iraq, iwapo itapatikana imani, utashi na ikhlasi ya kufanya hivyo, kwa hiyo inawezekana kutekeleza miradi mingi ya uzalishaji na kijamii”.

Akasema kua: “Kuna watu wanapigana na kujitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda nchi na kuna watu wanajenga, tunawaambia ndugu zetu katika mikoa mingine, hakika mradi huu sio kwa ajili ya kuleta ushindani na viwanja vingine bali ni kwa ajili ya kuchangia huduma zinazo tolewa na viwanja vingine, tuna muomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe kukamilisha mradi huu na tushuhudie utuaji wa ndege ya kwanza katika uwanja huu”.

Kisha baada yake aliongea rais wa kamati ya uzalishaji ya kitaifa na mkuu wa mkoa wa Karbala pamoja na spika wa bunge la mkoa, wote walizungumzia nafasi kubwa itakayo kua nayo uwanja huu utakapo anza kutumika, na kusisitiza umuhimu wa kufanya haraka katika utekelezaji wa mradi huu adhim.

Baada ya hapo zikaonyeshwa picha za majengo na ofisi za uwanja wa kimataifa wa Karbala, zilizo onyeshwa na dokta Nahidh Muhammad Swalehe rais wa kamati ya uongozi ya shirika la Copper chase watekelezaji wa mradi huu, na alielezea wasifu wa uwanja huu, na watu watakao changia katika utekelezaji, alisema kua; awamu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja huu itaghalimu kati ya milioni (2-4), kama kukiwa na mlundikano wa ndege na wa watu tutaupanua zaidi, sehemu itakayo jengwa jengo la wasafiri ina ukubwa wa mita za mraba (130,000). Katika awamu ya kwanza tutajenga katika mita za mraba (85,000), urefu wa eneo la uwanja ni kilometa (4.5) hili ni eneo kubwa sana linazidi daadhi ya maeneo ya viwanja vya kimataifa, ukiongeza na eneo la kusimama ndege, kutakua na sehemu nne za kusimama ndege katika hii awamu ya kwanza, jumla ya sehehu zote za kusimama ndege ni (12), mnara wa kuongoza ndege utakua ni miongoni mwa minara mirefu hapa Iraq na nchi zingine pia, utakua na urefu wa mita (60) pia kutakua na vituo vya kusimamia ndege.

Baada ya kumalizika kwa hafla ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulitoa pongezi kubwa kwa Atabatu Husseiniyya kutokana na mradi huu, wakawaombea mafanikio mema na wakamilishe haraka ili uweze kutumikia mji wa bwana wa mashahidi (a.s) na watu wanaokuja kumzuru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: